• This is Slide 1 Title

    This is slide 1 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 2 Title

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 3 Title

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Thursday, July 10, 2014

WEMA SEPETU, KAJALA MASANJA BIFF KUSHNEY!!



Muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu, amesema amefurahi kurudiana ‘ushosti’ na muigizaji mwenzake, Kajala Masanja, Wema alisema pamoja na Kajala kumkosea ila amefurahi kuwa naye karibu kwani alikuwa anakwazika na hasa alipokuwa anasikia habari zake kwa watu wa karibu na Kajala.
“Nashukuru Mungu hili bifu limeisha kiukweli, nimefurahi sana kwani nilikuwa nakwazika kila nikipata habari za Kajala kwa watu wake wa karibu, kiukweli nimefurahi,” alisema Wema.
Wema Sepetu na Kajala walikuwa na bifu lililokuwa linadhaniwa haliwezi kumalizika hadi kufikia hatua ya kuundwa kwa makundi yanayodaiwa ya kiuchochezi baina yao.

NEYMAR HOI, MUUGUZI AFUKUZWA





Muuguzi wa Hospitali ya Fortaleza Sao Paulo, Brazil  aliyopelekwa Neymar baada ya kuumia wakati wa mechi ya Brazil dhidi ya Colombia amefukuzwa kazi kwa kitendo chake cha kupiga picha za video wakati akiwasili hapo na kuzirusha kwenye mitandao ya kijamii. Picha hizo za video zilimwonyesha nyota huyo wa Brazil akipokelewa na kukimbizwa kwenye varanda za hospitali hiyo na madaktari zilionekana muda mfupi kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kutoka kwa taarifa kuwa Neymar hatoweza kucheza mechi zote zilizobaki za Kombe la Dunia.

Muuguzi huyo alijulikana kwa sababu mwisho wa video hiyo  aligeuza kamera upande wake na kusema “woo-hoo!” na kuonyesha tabasamu wakati nchi nzima ikiwa kwenye majonzi, pamoja na kushinda 2-1.
 Kwa mujibu wa Globo, uongozi wa hospitali umethibitisha kumfukuza muuguzi huyo kwa kitendo chake cha kuingilia maisha binafsi ya mgonjwa, wakati huohuo; Fifa haitochukua hatua yoyote dhidi ya beki wa Colombia aliyemuumiza Neymar, Fifa ilisema kamati ya nidhamu ilikaa na “hakuna haja ya kuchukua  hatua kwa tukio hilo’’ kwa sababu mwamuzi wa mechi hakuona wakati Camilo Zuniga akimgonga na kuchukua uamuzi kwa wakati


BRAZIL KIWANDA CHA SAMSUNG KUVAMIWA


Simu 40,000 na mali zenye thamani ya dola milioni thelathini na sita zaibiwa.

Huko Brazil kombe la Dunia likiendelea kurindima kiwanda cha kampuni ya simu aina ya Samsung chavamiwa na wezi huku takribani simu 40,000 , tarakilishi pamoja na vifaa vingine kuripotiwa vimeibwa na wezi hao. Majira ya usiku siku ya Jumatatu wezi walivamia kiwanda cha simu cha Samsung nchini Brazil na kuiba mali yenye thamani ya dola milioni thelathini na sita.
Kundi la wezi lililo vamia kiwanda hicho tayari lilikuwa limesha jihami na kujipanga vikali dhidi ya tukio hilo wafanyakazi wane waliokuwa wakitoka kazini walitekwa na kuporwa vitambulisho vyao ambavyo walivitumia kuweza kingie ndani kama wafanya kazi wa kiwandani hapo kilichopo  mjini Sao Paulo, kutokana na kujipanga kwa kundi hilo la wezi imeripotiwa kuwa waliwazidi nguvu walinzi na kutumia muda wa saa tatu kufanya uhalifu.
Polisi wanasema kuwa genge hilo lilikuwa na wezi, 20 ambao walifanikiwa kuiba simu 40, 000 pamoja na tarakilishi, tabiti na vifaa ningine vyenye thamani ya dola milioni 36, walipovamia kiwanda hicho waliamuru wafanyakazi wote kuondoa betri zao kwenye simu ili wasiweze kumpigia mtu yeyote simukitendo kilichowaruhusu kutumia masaa matatu kufanya uhalifu huo na walifahamu vyema ambako vifaa vyenye thamani zaidi vilipokuwa vimewekwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa na kwamba kampuni hiyo haina tatizo lolote kwa sasa.Polisi wanachunguza kanda za video kuona ikiwa wanaweza kuwatambua wezi hao.

WATAFITI SOMALIA, UHARAMIA HUENDA UKAPUNGUA!



Utafiti wa hivi karibuni unaashiria kwamba uharamia kutoka pwani ya Somalia huenda ukapungua kwa kiwango kikubwa kwa kuwapatia wazee wa koo za kisomali njia mbadala za kujikimu kimaisha. Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo wa chuo kikuu cha Oxford na King's College mjini London, iliyochapishwa katika jarida moja la Uingereza, Jamii huwalinda maharamia wakati hawana njia nyengne za kujipatia kipato.
Kwa sasa Jamii ya kimataifa inategemea mikakati iliyo ghali mno, zikiwemo meli za kijeshi kuzuia uhaharamia wa majini na kuweka njia za safari za majini kuwa salama .
Lakini utafiti huu unakubaliana na yale ambayo yamekuwa yakipendekezwa na wadau mbalimbali Afrika mashriki, kwamba suluhu la kudumu ni kujenga miundo mbinu kama vile bandari na barabara zitakazo wawezesha wanavijiji wa koo mbalimbali wanufaike kwa fursa za kibiashara halali, zitakazowawezesha kupata tiza za kuendeleza maisha yao.

JAJI MUTUNGI APEWA TAHADHARI NA CHADEMA MTWARA



Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi apewa tahadhali kali na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mtwara, kuacha  kukiingilia chama katika katiba yake kwa kutoa taarifa zenye lengo hasi kwa maendeleo na ukuaji wa demokrasia nchini
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo mkoani mtwara, Kasim Bingwe alisema Jaji Mutungi kukiingilia chama hicho katika shughuli zake za halali ni kinyume na majukumu ya ofisi yake kwa mujibu wa sheria na matarajio ya wananchi katika kujenga demokrasia nchini.
“Msajili anatambua kuwa huu ni ubakaji wa demokrasia na pia anaendelea kutolea hoja mambo yasiyo na mashiko huku akinyamazia mambo yanayolalamikiwa kukwaza demokrasia nchini, licha ya msajili kudai amepokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA wakiwemo waliofukuzwa, iweje ayatoe leo kwenye vyombo vya habari huku akijua kuwa kifungu kinacholalamikiwa kilifutwa na katiba mpya ya 2006?” alihoji.
Mwenyekiti  huyo wa chama cha demokrasia na maendeleo mheshimiwa Bingwe aliongezea kwa kusema:
 “Hivi msajili ameshindwa kuona kuwa wanachama wa chama cha CCM wameanzisha na kuendeleza kampeni za uchaguzi wa 2015 kabla ya wakati huku akijua kuwa hilo ni kinyume cha Katiba na sheria ya uchaguzi?.....inaonekana msajili haoni vijembe vya makundi ndani ya CCM kugombea uongozi kwenye chama chao kabla hata ya muda jambo lililosababisha baadhi yao kuadhibiwa.
Anaongeza kuwa kitendo cha msajili kutamka kuwa mazuio kwa uongozi wa CHADEMA kujihusisha na mambo ya chama kumezua mtafaruku miongoni mwa wanachama na miongoni mwa wapenda chama, hivyo kuwaweka katika hali tete.
“Jambo hili limetusababishia usumbufu wa kujibu mambo yasiyo na tija kwa jamii huku tukiacha kutekeleza majukumu ya ndani ya chama na jamii katika ujenzi wa demokrasia na uchumi wa jamii,” alisema Bingwe.
Hivi karibuni msajili alinukuliwa akizungumza na vyombo vya habari akikaripia na kuwazuia viongozi wakuu wa Chadema kutogombea tena nyadhifa zao, kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja katiba ya chama hicho.