Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ameunda kamati ndogo yenye ujumbe
wa watu 10 kwa ajili ya kushughulikia masuala ambayo hayakufikia muafaka
wakati wa majadiliano ya kupitia sura mbalimbali za Rasimu ya Katiba Mpya
kwenye Kamati 12 za Bunge hilo.
Kamati
hiyo itakuwa inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samia Suluhu
Hassan,ambapo wajumbe wa kamati hiyo wametoka kila pande ya
Muungano yaani watano wametoka Tanzania Bara na watano kutoka Zanzibar.
Aidha Mhe.
Sitta akizungumzia kuhusu maendeleo ya kazi za Kamati hizo,
ambapo alisema zinaendele vizuri, hivyo kuanzia wiki ijayo sura zote 15
zitakuwa zimepigiwa kura,hivyo Kamati hizo zitakuwa zimemaliza sura 17 ya
rasimu hiyo na za nyongeza ifikapo Agosti 27,mwaka huu ili kuanza
kuwasilisha katika Bunge hilo kuanzia Septemba 2,mwaka huu.
Hayo
yalisemwa leo na Mhe. Samuel Sitta wakati akizungumza na waandishi wa
habari alipokutana nao leo kuhusu muhtasari wa kikao cha Kamati ya Uongozi wa
Bunge hilo kilichokaa leo kutathmini kazi za Kamati 12 za Bunge hilo
lilipofikia pamoja kuridhia baadhi ya mapendekezo ya kuongeza Ibara na sura
ndani Rasimu ya Katiba katika Kamati zao.
Mwenyekiti
huyo aliyataja mambo ambayo yatashughulikiwa na kamati hiyo, ni muundo wa
Bunge katika masuala ya Muungano, uraia pacha, mahakama ya
kadhi na kamati ya pamoja ya fedha.
“Haya
mambo manne nimeagiza ufanyike utaratibu maalum,” alisema Mhe. Sitta.
Mhe
. Sitta akizungumzia kuhusu tathimini ya mwenendo wa Kamati hizo, alisema
zipendekeza masuala kadhaa na kuacha mengine kama yalivyo katika rasimu
hiyo.
Akizungumzia
kuhusu yaliyojadiliwa katika kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo,kabla ya
kukutana na waandishi wa habari, Mhe. Sitta alisema kamati hiyo imepokea
mapendekezo kutoka katika kamati mbalimbali kuhusu kuongezeka kwa sura na Ibara
za rasimu hiyo.
Aliyataja
mapendekezo hayo , likiwemo la Tume ya Marekebisho ya Katiba
lililowasilisha na Jaji Warioba kuhusu ardhi, mazingira na rasilimali za taifa,
Jumuia ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT) na pendekezo la Haki
ya Watumiaji huduma na bidhaa ili kuwalinda walaji lililowasilishwa , Hawa
Ng’umbi ambaye ni mjumbe wa Bunge hilo.
Aliyataja
mapendekezo mengine ni la Jukumu la Serikali kujenga
uchumi imara, ambapo lengo ni kuwa na maendeleo ya uchumi wa ujamaa na
kujitegemea na Kuwepo kwa Baraza la Habari, la wajumbe wa 201 kuhusu ardhi,
wafugaji, wavuvi pia na wachimbaji wadogo ili ziweze kutungwa Sheria za
kusimamia masuala hayo.
Mhe. Sitta
alisema kutokana na mapendekezo hayo kutakuwepo na ongezeko la
ukurasa na sura kadhaa katika rasimu hiyo.
Alisema
Kamati imebaini tatizo la mahudhurio, aliwapongeza wajumbe wa Bunge hilo
kutoka upande wa Zanzibar kwa kuwa na mahudhurio mazuri kwenye vikao kuliko
kutoka Tanzania Bara kuacha visingizio vya kutohudhuria vikao.
Katika
hatua nyingine Mhe. Sitta alisema kutakuwepo na wataalamu kabla ua
kumalizika kwa wiki hii kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa mambo
kadhaa kutoka Hazina kwa pande zote za Muungano, ambapo ataukuwepo pia Gavana
wa Benki Kuu, Profesa Bonaventure Rutinwa kwa ajili ya suala la uraia pacha,
uhamiaji na Profesa Issa Shivji ambaye ataoa ufafanuzi juu ya aina ya
Muungano ili kuwa na uwiano kwa kuwa hivi sasa yapo mambo machache. Imeandikwa na
Magreth Kinabo, Dodoma
0 comments:
Post a Comment