• This is Slide 1 Title

    This is slide 1 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 2 Title

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 3 Title

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday, April 23, 2016

Watumishi HEWA Wakopa Mamilioni ya Pesa Benki; Kilimanjaro



Msako ulioanzishwa na Rais John Magufuli wa kutokomeza tatizo la wafanyakazi hewa katika utumishi wa umma, umeendelea kuibua mazito, ambapo mkoani Kilimanjaro, Benki ya CRDB imejikuta ikitoa mkopo kwa waliokuwa wafanyakazi hewa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Helga Mchomvu aliyasema hayo akidai kuwa, yamegundulika baada ya Serikali kuunda kamati za uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 500 katika halmashauri hiyo.

Kabla ya kuibuka kwa kisa hicho kinachoonesha namna wafanyakazi hewa alivyokuwa wakiibia nchi, hivi karibuni mkoani Singida, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Imani Nyamangaro, alipandishwa kizimbani akidaiwa kujilipa mishahara ya wastaafu 57, yenye thamani ya Sh milioni 29.4.

Mbali na mhasibu huyo, Rais Magufuli alipokuwa mapumziko kijijini kwake Mlimani, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, alieleza kisa kingine kilichoshitua jamii kuwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), kulikuwa na mtumishi mmoja ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17.

Benki ya CRDB Hai

Akizungumza jana, Mchomvu alidai kuwa watumishi watatu wa halmashauri hiyo; wawili wa Idara ya Utumishi na mmoja Mchumi, walikopa katika Benki ya CRDB Sh milioni 35.2, kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu Idara ya Utumishi na Utawala, Gudila Mashele, Ofisa Utumishi Daraja la Kwanza, Faraja Ndatu na Mchumi Daraja la Pili, Isaiah Bayege. 

Kutokana na tuhuma hiyo iliyoibuliwa na kamati hizo za uchunguzi, Mchomvu alisema Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, limewafukuza kazi watumishi hao.

Mbali na tuhuma ya kujipatia mkopo kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa, Mchomvu alisema kuna watumishi wengine wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za wizi wa fedha za muda wa kazi wa ziada wa madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Machame wilayani hapa, huku mwingine akifukuzwa kwa kununua dawa hewa za hospitali hiyo.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mhasibu Daraja la Kwanza, Edwin Kalokola na Mhasibu Msaidizi, Valentina Elisha, wanaodaiwa kuiba Sh milioni 24.4 za muda wa kazi wa ziada wa madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo.

Mbali na wahasibu hao, yupo pia dereva Derick Urassa, aliyefukuzwa kwa tuhuma za kushiriki katika ununuzi wa dawa hewa katika hospitali hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 32.7. 

Walioshushwa cheo 
Alisema wapo pia watumishi walioshushwa vyeo kutokana na tuhuma mbalimbali, ikiwemo kughushi nyaraka na kuidhinisha malipo bila idhini ya mwajiri.

Miongoni mwao ni pamoja na Ofisa Muuguzi Msaidizi Daraja la Kwanza, Agness Chami na Katibu wa Afya Daraja la Kwanza, Gilbert Mashamba.

Wengine ni wahasibu waandamizi wawili, Kasisim Herpa na John Bogohe na Mhasibu Daraja la Kwanza, Christopher Manzi, ambao wanatuhumiwa kuidhinisha malipo mbalimbali ya Sh milioni 488.2, bila kuwa na idhini kinyume na taratibu za kazi.

Walivyobambwa
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Saidi Mderu alisema tuhuma hizo ziligunduliwa na Mkaguzi wa Ndani wa halmashauri hiyo, Michael Mosha na kufanyiwa kazi na tume hizo zilizoongozwa na Katibu Tawala Msaidizi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Makiluli.

Baada ya kubainika kwa tuhuma hizo, Mderu alisema baraza hilo lilimpongeza mkaguzi huyo kwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwa kuwa angeweza kudanganyika kutumia fedha hizo.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa, amepongeza baraza hilo kwa hatua hizo na kueleza kuwa kazi kubwa ya madiwani ni kusimamia mali na rasilimali za Serikali, ili wananchi wapate huduma bora za Serikali yao ya Awamu ya Tano ambayo ina dhamira ya kuwahudumia.

BAN KI-MOON AMBANA MACHAR KIREJEA JUBA

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Ijumaa (22.04.2016) amemuwekea mbinyo zaidi kiongozi wa waasi nchini Sudan kusini Riek Machar kurejea mjini Juba "bila kuchelewa" na kuanza kazi katika serikali ya mpito.

Kiongozi wa waasi Sudan kusini Riek Machar

Machar alitarajiwa kurejea katika mji mkuu siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa makubaliano ya kisiasa yenye lengo la kumaliza vita vya miaka miwili, lakini tofauti kuhusiana na mipango ya kiusalama mjini Juba inachelewesha kurejea kwake.

Ban amesema serikali ya rais Salva Kiir imekubali pendekezo la muafaka kuhusiana na matayarisho ya kurejea kwa Machar na kusema hatua hii inapaswa kusaidia kuundwa kwa haraka kwa serikali mpya ya umoja wa kitaifa.

Makamu wa rais mtarajiwa Riek Machar wa Sudan kusini

"Kuendelea na hali ya ushirikiano itakuwa muhimu wakati viongozi wa nchi hiyo wakianza mchakato wa kubadilisha miaka ya uharibifu uliosababishwa na mzozo huo kwa watu wa Sudan kusini," amesema katika taarifa.

Mateso ya watu wa Sudan kusini

Ban amemtaka Machar kusafiri kwenda Juba " bila masharti zaidi" hali ambayo inaweza kuchafua mchakato wa amani na kuendeleza hali ya mateso yanayowakuta watu wa Sudan kusini."

Chini ya makubaliano ya amani, Machar alitakiwa kurejea tena katrika wadhifa wake wa makamu wa rais katika serikali mpya itakayodumu kwa muda wa miezi 30 na kuielekeza nchi hiyo katika uchaguzi mkuu.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon

Kikwazo cha hivi sasa kinahusiana na idadi ya bunduki na vifaa vya kufyatulia maguruneti ambavyo vikosi vya waasi vinavyomlinda Machar vitaruhusiwa kuwa navyo.

Vita vya Sudan kusini vilianza Desemba mwaka 2013, wakati Kiir alipomshutumu Machar kwa kula njama za kumpindua. Mzozo huo umeweka wazi mpasuko wa tofauti za kikabila na umekuwa ukionesha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na ubakaji wa makundi, uchomaji moto vijiji na hata ulaji nyama za watu.

Ombi la Marekani

Kwa ombi la Marekani, baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana siku ya Jumatatu na kuelezea "wasi wasi wake mkubwa " kwa kushindfwa kurejea Machar mjini Juba.

Rais wa Sudan kusini Salva Kiir (kulia)

Jumuiya zenye nguvu duniani, ikiwa ni pamoja na Umoja Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya , China , Uingereza na Marekani , zimewapatia Machar na Kiir muda wa mwisho hadi leo Jumamosi (23.04.2016) kutatua tofauti zao.

Mamia kwa maelfu ya watu wameuwawa na zaidi ya watu wengine milioni mbili wamelazimika kuyakimbia makaazi yao tangu vita hivyo vilipozuka Desemba mwaka 2013.

Wasiwasi unatuwama katika hali ya kutoaminiana kuhusiana na silaha hali ambayo imechelewesha kurejea kwa Machar.

Wanajeshi wa jeshi la serikali ya Sudan kusini

Kikosi cha wanajeshi waasi wapatao 1,370 tayari kimewasili mjini Juba kama sehemu ya makubaliano ya amani wakati majeshi ya serikali yanasema yameondoa wanajeshi wake wote isipokuwa wanajeshi 3,420 , kwa mujibu wa makubaliano. Wanajeshi wengine wote wanapaswa kubakia kiasi ya kilometa 25 nje ya mji mkuu.

Katika moja kati ya kambi tatu za waasi mjini Juba, waasi wanatengana na kambi ya majeshi ya serikali kiasi ya mwendo wa miguu wa dakika tano na wanaweza kuonana na karibu iwapo kutatokea rabsha zozote.

Siri ya herufi ya mwanzo ya Jina lako

Je Unajua Siri ya herufi ya mwanzo ya jina lako?. Soma hapa utaweza kuelewa Tabia zako au tabia za rafiki au mpenzi wako.

>HERUFI A
>Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira. Herufi A inawakilisha Nyota ya Punda.
>HERUFI B
>Mwenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake. Herufi B inawakilisha Nyota ya Ngombe,
>HERUFI C
>Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano Herufi C inawakilisha Nyota ya Mapacha,
>HERUFI D
>Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo. Herufi C inawakilisha Nyota ya Kaa,
>HERUFI E
>Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu. Herufi E inawakilisha Nyota ya Simba,
>

CANADA KUMTIA KIZUIZINI MWANAFUNZI WA SUDAN KUSINI

Wakuu wa Canada wanasema wamemuweka kizuizini mwanafunzi wa shule ya sekondari kutoka Sudan Kusini, kwa sababu wanaamini ana umri wa miaka 29 na siyo 16, kama aliyvodai alipoingia nchini.

Jonathan Nicola anasemekana alikuwa mchezaji mzuri wa mpira wa kikapu, katika timu ya shule yake ilioko Windsor, Ontario.

Maafisa wa mpakani, wanasema mwaka jana, paspoti ya Jonathan Nicola, ilionesha kuwa alizaliwa 1998, lakini ombi lake la visa ya kuingia Marekani, lilionesha chapa yake ya kidole, ilifanana na mtu aliyezaliwa 1986.

Sasa anaweza kufukuzwa nchini.

MAKUBALIANO YA SYRIA MATATANI

Rais Barack Obama wa Marekani pamoja na mjumbe wa Umoja wa mataifa nchini Syria Staffan Di Mistura wamesema kuwa wanahofia kwamba makubaliano ya Syria huenda yakaanguka.

Katika ghasia za hivi karibuni,watu 18 wamefariki kufuatia mashambulio ya serikali mjini Aleppo huku ndege moja ya kivita ya Syria ikidaiwa kuanguka karibu na mji wa Damascus.

Akizungumza mjini Geneva ,Mistura amesema kuwa alitaka kuitisha mkutano wa kijimbo ili kunusuru makubaliano hayo.

Amesema kwamba watu 400,000 huenda wamefariki katika mzozo huo.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa hana ushahidi wa idadi hiyo lakini akaongezea kuwa inakaribia