• This is Slide 1 Title

    This is slide 1 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 2 Title

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 3 Title

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Thursday, March 26, 2015

WAGOMBEA WAAHIDI UCHAGUZI KUFANYIKA KWA AMANI NIGERIA



Wagombea wawili wa uchaguzi wa urais nchini Nigeria wameahidi kufanyika kwa uchaguzi wa amani,na kuongezea kuwa wataheshimu matokeo ya uchaguzi ulio huru na haki.
Rais Goodluck Jonathan pamoja na mpinzani wake wa karibu Muhammadu Buhari,pia wamewataka wafuasi wao kuiga mfano huo.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi baada ya kuahirishwa mwezi uliopita.
Mwandishi wa BBC amesema kuna wasiwasi kuhusu iwapo tume ya uchaguzi imejianda kusimamia uchaguzi huo na iwapo shughuli hiyo itaafikia matarajio ya wengi.

NDEGE ILIYO ANGUKA UFARANSA, ILIANGUSHWA MAKUSUDI



Rubani wa ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya jumanne alitaka kuiharibu ndege hiyo kulingana na maafisa wa Ufaransa.Kiongozi wa mashtaka katika mji wa Mersaille ,Brice Robin, akizungumza kulingana na habari aliyopata katika kijisanduku cha kunasa sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa ndani ya chumba cha kuendesha ndege pekee.


Rubani huyo kimakusudi aliishusha ndege hiyo kwa kasi huku rubani mwenza akiwa nje ya chumba hicho cha kuendesha ndege.
Bwana Robin amesema kuwa kulikuwa na kimya kikubwa ndani ya chumba hicho wakati rubani mwenza alipojaribu kuingia kwa nguvu.
Hatahivyo abiria walisikika wakipiga nduru kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo,aliongezea.
 
Rubani huyo kwa jina Andreas Lubtiz,mwenye umri wa miaka 28, alikuwa hai hadi wakati ndege hiyo ilipoanguka ,kiongozi wa mashtaka alisema.


Ndege hiyo aina ya Airbus 320 iliokuwa ikitoka Barcelona kuelekea Duesseldorf Ujerumani iligonga mlima na kuwauwa abiria wote 144 pamoja na wafanyikazi sita wa ndege baada ya kushuka kwa dakika nane.
"Tunasikia rubani akimuuliza rubani mwenza kuchukua udhibiti wa usukani wa ndege hiyo na vilevile tunasikia sauti ya kiti kikisonga nyuma na mlio wa mlango ukifungwa,bwana Robin aliwaeleza wanahabari.

UFISADI:KENYATTA AWASIMAMISHA 175



 Mawaziri 5, makatibu 6 wa kudumu na Magavana 10 wametajwa miongoni mwa maafisa 175 wa umma watakaolazimika kunga'atuka mamlakani katika siku 60 zijazo iliuchunguzi wa kina ufanyike kuhusu madai ya ufisadi dhidi yao. Hayo yalibainika katika ripoti iliyotolewa bungeni na rais Uhuru Kenyatta katika kikao maalum cha bunge la taifa kilichowajumuisha wabunge na maseneta.
Rais Kenyatta aliwataka maafisa wote wa umma waliotajwa katika ripoti hiyo waondoke ilituhuma zote dhidi yao zichunguzwe kwa kina na tume ya kupambana na ufisadi.
''Kwa hakika imewadia wakati ambapo serikali yangu haina budi ila kuchukua hatua mahsusi ambayo inalenga kukomesha hili zimwi la ufisadi mara moja''

UFISADI ''Ufisadi umevuka mipaka na lazima nasi tujifunge kibwebwe na kukabiliana nao''.
''Natarajia kuwa wale waliotajwa katika ripoti hii watanga'tuka mamlakani hadi pale uchunguzi utakapokamilishwa ndipo warejee afisini.'' alisema Kenyatta.
Kenyatta aliongezea kusema kuwa ''Ninamtaka kiongozi wa mashtaka ya umma kuanzisha uchunguzi mara moja kuhusiana visa vyote vilivyotajwa humu katika kipindi cha siku 60 zijazo''.


Ripoti hiyo iliyotayarishwa na tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya KACC inawadia wakati ambao kumekuwa na visa vingi vya ufisadi haswa katika serikali kuu na pia serikali za majimbo.
Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Kisa kilichozua mjadala ni kile cha 'Anglo Leasing'' ambayo ilijumuisha kandarasi za idara ya Uhamiaji idara ya upelelezi na Idara ya usalama wa taifa.
Mabilioni ya fedha yalilipwa kwa wanakandarasi waliotarajiwa kuwasilisha kazi ambazo hazikuwahi kufanyika hata wa leo.
Magavana 10 kati ya 47 wametajwa katika ripoti hiyo ambayo itatangwwa rasmi siku ya jumanne katika mabunge yote mawili.
Duru zinasema kuwa Kamati nzima ya bunge inayochunguza ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma imetajwa katika ripoti hiyo.
 MSAMAHA
Aidha Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Kenyatta alisema''ili wakenya waweze kusonga mbele na kusahau yaliyopita kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali zilizotangulia ni wajibu wangu
kuchukua fursa hii na kuwaomba msamaha wote waliodhulumiwa kwa njia moja au nyengine.
Zaidi ya Wakenya 650,000 walifukuzwa makwao kufuatia vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2008 na tume maalum ya haki ukweli na maridhiano TJRC
ilipendekeza kuwa sharti serikali iombe radhi kwani fedha haziwezi kufuta machungu ya mateso ambayo wakenya wamepitia''
''Hata hivyo licha ya mapendekezo ya tume hiyo ya maridhiano,nimeagiza wizara ya fedha itenge shilingi bilioni 10 dola milioni 110, katika kipindi cha miaka
mitatu ijayo kwa ajili ya kuwafidia wale wote walioathirika''

TAMASHA LA MUZIKI KENYA



Nchini Kenya, ni wakati wa tamasha la sanaa ambapo shule na vyuo vinashindana.
Maelfu ya wanafunzi hukusanyika kuonesha vipaji vyao katika sanaa za utamaduni.
Muhimu tu washinde tuzo. Na si rahisi kwani wavulana ni wasichana na wasichana ni wavulana.