Moja kati ya mikosi anayo kutana nayo Chris Brown ni kukumbana na
matatizo ama shutuma za ugomvi na watu tofauti tofauti.. leo Hi5 Anzisha kitovu
cha habari kimenasa jipya, hivi karibuni Chris Brown Hit maker wa “LOYAL” ameripotiwa
kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu bibie Karrueche Tran, kama ilivyo pale
mahusiano yanapo vunjika basi kila mmoja anachukua chake na kurudisha walivyo
peana ndicho kilichotokea kwa wapendanao hawa Chris Bwown na mwenziwe Karrueche
baada ya kuachana kila mmoja aka delete picha za mwezie kwa instagram na
mitandao mingine waliyo kuwa wamepost picha zao pindi wako katika penzi zito. Kwa
mujibu wa chanzo chetu cha habari kuacha na kurudiana ndio mchezo wa wapenzi
hawa kweli wagombanao ndio wapatanao.