Ahadi ya Rais Barak Obama,
Kuimarisha Ulinzi Marekani.
Kitengo cha sheria nchini Marekani
kimeanza kufanya uchunguzi wa jinai dhidi ya kifo chamwandishi wa habari mwenye
asili ya Marekani ,James Foley aliyeuawa na wapiganaji wa kiislamu wenye
msimamo mkali. Mwanasheria mkuu wa kitengo hicho,Eric Holder ameweka wazi kuwa
wote waliohusika na mauaji ya mwandishi huo watawatia mkononi muda si mrefu. Maofisa
wa serikali ya Marekani wandai kwamba askari hao wauaji walidai kiasi kikubwa
cha pesa zipatazo dola za kimarekani zaidi ya milioni mia moja na thelathini
kama fidia ya kumuachilia James Foley.
Marekani imekwisha anza harakati za
kuwasaka na hatimaye kuwakamata waliohusika na mauaji ya mwandishi huyo kwa
kurusha ndege zake takriban sita katika anga inayomilikiwa na waislamu
kaskazini mwa Iraq.pamoja na kwamba waislam hao kutishia kumuua mmarekani
mwingine wanayemshikilia kama ulipizaji wa kisasi endapo mashambulio yataelemea
upande wao.
0 comments:
Post a Comment