Boko Haram wazidi kumlaza macho Raisi Jonathan Moyo
Kundi la wapiganaji la kiislam la Boko Haram,wamevamia shule
moja ya mafunzo ya kipolisi kilichoko kwenye kitongoji cha Gwoza karibu na
mpaka wa nchi ya Cameroon ambacho hufundisha maofisa wa Polisi nchini Nigeria.
Kikundi hicho cha Boko Haram pia kinasemekana kuudhibiti mji wa jirani na
Gwoza uitwao Buni Yadi, shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights
Watch wametoa takwimu ya vifo vilivyosababishwa na kundi hilo kuua watu zaidi
ya elfu kumi mpaka sasa tangu walipoanzisha harakati za kutaka upande wa
kaskazini mwa Nigeria uwe chini ya utawala wa Kiislam.
0 comments:
Post a Comment