Hivi
karibuni Hi5 Media chini ya tawi la Video Production ya Akonshaz Music, Visualized
EFX jijini Dar es Salaam waandaaji wa kazi mbalimbali zinazo jumuisha video ama
vichupa kama lugha ya vijana wengi wengi wa kisasa wasemavyo wana tarajia
kuangusha mzigo wa filamu fupi inayohusu maisha ya mtaa yalivyo. Akiongea na
Bloger wetu muigizaji kinara katika filamu hii fupi Joeseph Kanyopa al maarufu
kama Kanyo Mc azungumzia juu ya ujio wa kazi yake iliyo pewa jina la SADALI kwa
mara ya kwanza katika tasnia ya filam Tanzania, licha ya kuwa ndiyo kazi yake
ya kwanza kuifanya anategemea ushauri na mawazo chanya kutoka kwa wadau watakao
pata kuiona filamu ya Sadali.
Bloger
wetu pia alipata nafasi ya kuongeea na Director wa filamu hiyo ya Sadali pia
ndiye Mkurugenzi wa Visualized EFX Creyz Beez kwa upande wake alizungumzia
ugumu alioupata wakati wa kuiongoza filamu ya Sadali. “Kushuti filamu
kunahitaji maandalizi marefu sana lakini sicho kilichofanyika katika filamu hii
na imetokana na kwamba tulikuwa tunahitaji kuona katika upande wa filamu
matatizo ni yapi mbali na hilo muandaaji wa script hakuwasilisha script so ili
bidi tufanye kazi kutegemea story board, mengine ni ya kawaida tu msanii
kukosea mara kwa mara, kuchelewa kufika Location lakini kimefanyika kitu kizuri na ndio ujio
wa Visualized EFX”. Kupitia Mtandao mpana wa Hi5 Media baada ya Filamu ya
Sadali kutoa itapatika katika touvuti yetu ya YouTube, pia itapatikana katika
blog yetu, nikuambie tu Visulized EFX imesha Anzisha kama wasemavyo Hi5 Media
stay Tune.
Picha hizi ni snap shot za baadhi ya scene zilizomo ndani ya filamu ya Sadali.