Hivi ndivyo jamii ya
kitanzania inavyo jilea maika ya sasa huku shutuma nyingi zikielekezwa katika
matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii pasi na kuchunguza nini chanzo ama
sababu kubwa inayo pelekea jamii yetu yakitanzania kusahau maadili yetu. Tuanze
na kujiuliza hivi ni kwanini maadili yana momonyoka kila leo, zamani enzi za
mababu zetu si kwamba hakukuwa na maadili mabovu lakini kulingana na kwamba
utandawazi umeifanya dunia kuwa kijiji mengi yanayofanyika kwa siri sasa hayana
sehemu yakufichwa. Moja kati ya jinsia inayo jaliwa sana karibu kwa kila sekta
ni jinsia ya kike na si kwa Tanzania tu hii ni sera ya dunia nzima lakini dada
zetu ama mabinti wa kiafrika hususani wakitanzania wamekuwa wakijishusha hadhi
na heshiama wanazopewa katika jamii kwa mambo wanayo fanya sasa, kabla hatuja
anza kugusia yanayo endelea kwenye mitandao sasa mpendwa msomaji wangu nikujuze
jambo moja kwanza, kabla ya hata mabinti hawa wachache kuanza kutupia ndani zao
nje walianza na mavazi yasiyo stahili ambayo yanaweka karibu robo tatu ya mwili
nje sasa kila jambo huanza likiwa dogo tukaanza kuona post mbalimbali za picha
zao za wilu (utupu) zikiwa hadharini eti zimeliki wengine wapenzi wao wamezitoa
kisa wameachana mpaka sasa wana amua wenyewe kujipiga na kuziweka kwenye
mtandao.
Ona jinsi mzunguko
ulivyo unamiliki simu yenye uwezo mzuri wa kupiga picha kisha simu hiyo ina
apps tofauti za kimtandao zinazo ruhusu kufanya system data uploading hapa namaanisha Instagram, whattsapp, facebook
ambapo baada yakujipiga picha ukiwa ndani kwako then mtu huyo anapost picha
hizo kwa mtandao alafu baadae tuseme zimeliki au mmoja amezivujisha. Muda
mwingine bishara nayo huitaji matanazo ili iweze kutoka sasa tuangali je ni
kosa la mtandao au watumiaji wenyewe maana mtandao huohuo unamfanya mtumiaji
kufaulu huko mavyuoni kwa kusafu material mbalimbali na ndio mtandao huohuo
unaofanya mtumiaji kupost picha zake za utupu. Pengine ni uhuru binafsi wa
matumizi haya ya mtandao au ni kuto kuwepo na mfumo wauzuizi wa vitu vya kuonekana kwenye mtandao,
pia hili halifatiliwi sana kwa maana wako wakubwa ama wanene wanopenda kuona
vitu hivyo ili wajue wapi pa kuchepukia. Amini kitu kimoja katika namba
ikipungua au kuongezeka moja basi mahesabu hayawi sahihi sasa hata haya tunayo yaona
au kuonekana kwenye mtandao ya athiri sana jamii yetu na kuipeleka kusiko
sahihi.
0 comments:
Post a Comment