Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,
Jaji Francis Mutungi apewa tahadhali kali na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Mkoa wa Mtwara, kuacha kukiingilia
chama katika katiba yake kwa kutoa taarifa zenye lengo hasi kwa maendeleo na
ukuaji wa demokrasia nchini
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia
na maendeleo mkoani mtwara, Kasim Bingwe alisema Jaji Mutungi kukiingilia chama
hicho katika shughuli zake za halali ni kinyume na majukumu ya ofisi yake kwa
mujibu wa sheria na matarajio ya wananchi katika kujenga demokrasia nchini.
“Msajili anatambua kuwa huu ni
ubakaji wa demokrasia na pia anaendelea kutolea hoja mambo yasiyo na mashiko
huku akinyamazia mambo yanayolalamikiwa kukwaza demokrasia nchini, licha ya msajili
kudai amepokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA wakiwemo waliofukuzwa, iweje
ayatoe leo kwenye vyombo vya habari huku akijua kuwa kifungu kinacholalamikiwa
kilifutwa na katiba mpya ya 2006?” alihoji.
Mwenyekiti huyo wa chama cha demokrasia na maendeleo
mheshimiwa Bingwe aliongezea kwa kusema:
“Hivi msajili ameshindwa kuona kuwa wanachama
wa chama cha CCM wameanzisha na kuendeleza kampeni za uchaguzi wa 2015 kabla ya
wakati huku akijua kuwa hilo ni kinyume cha Katiba na sheria ya uchaguzi?.....inaonekana
msajili haoni vijembe vya makundi ndani ya CCM kugombea uongozi kwenye chama
chao kabla hata ya muda jambo lililosababisha baadhi yao kuadhibiwa.
Anaongeza kuwa kitendo cha msajili
kutamka kuwa mazuio kwa uongozi wa CHADEMA kujihusisha na mambo ya chama
kumezua mtafaruku miongoni mwa wanachama na miongoni mwa wapenda chama, hivyo
kuwaweka katika hali tete.
“Jambo hili limetusababishia
usumbufu wa kujibu mambo yasiyo na tija kwa jamii huku tukiacha kutekeleza
majukumu ya ndani ya chama na jamii katika ujenzi wa demokrasia na uchumi wa
jamii,” alisema Bingwe.
Hivi karibuni msajili alinukuliwa
akizungumza na vyombo vya habari akikaripia na kuwazuia viongozi wakuu wa
Chadema kutogombea tena nyadhifa zao, kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja katiba
ya chama hicho.
0 comments:
Post a Comment