Utafiti wa
hivi karibuni unaashiria kwamba uharamia kutoka pwani ya Somalia huenda
ukapungua kwa kiwango kikubwa kwa kuwapatia wazee wa koo za kisomali njia
mbadala za kujikimu kimaisha. Kwa
mujibu wa ripoti ya utafiti huo wa chuo kikuu cha Oxford na King's College
mjini London, iliyochapishwa katika jarida moja la Uingereza, Jamii huwalinda
maharamia wakati hawana njia nyengne za kujipatia kipato.
Kwa sasa Jamii ya kimataifa
inategemea mikakati iliyo ghali mno, zikiwemo meli za kijeshi kuzuia uhaharamia
wa majini na kuweka njia za safari za majini kuwa salama .
Lakini utafiti huu unakubaliana na
yale ambayo yamekuwa yakipendekezwa na wadau mbalimbali Afrika mashriki, kwamba
suluhu la kudumu ni kujenga miundo mbinu kama vile bandari na barabara zitakazo
wawezesha wanavijiji wa koo mbalimbali wanufaike kwa fursa za kibiashara
halali, zitakazowawezesha kupata tiza za kuendeleza maisha yao.
0 comments:
Post a Comment