Wizara ya
ulinzi inasema ndege hiyo ilikuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa
Luhansk, Maafisa wa Ukraine wanasema watu wanaopigana kujitenga na
kujiunga na Russia, wametungua ndege ya uchukuzi ya kijeshi na kuuwa watu
wote 49 waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Ofisi ya mwendesha mashataka mkuu huko
Ukraine, ilisema wanajeshi 40 na wafanyakazi tisa waliuawa mapema leo
Jumamosi baada ya ndege hiyo ya jeshi la angani la Ukraine kupigwa risasi
na kuanguka. Wizara ya ulinzi inasema ndege hiyo ilikuwa ikikaribia kutua
katika uwanja wa ndege wa Luhansk ilipopigwa risasi. Ukanda wa video
unaonyesha mlipuko mkubwa karibu na uwanja huo wa ndege, unaoaminika kutoka kwa
ndege hiyo.
0 comments:
Post a Comment