WAWILI KUWAHISHWA HOSPITALI WAKIWA
MAJERUHI
Watu wanne wameripotiwa kuuwawa asubuhi ya Jumatano baada ya ndege ya mizigo
kuanguka katika mtaa wa Utawala mjini Nairobi na kusababisha uharibifu wa
majengo mawilli kabla ya ndege hiyo kuanza kuwaka moto
Mbali na ndege hiyo kusababisha vifo vya watu wanne waliokuwa ndani ya ndege
hiyo akiwemo na rubani aliye kuwa akipaisha ndege hiyo chanzo cha habari
kinaeleza kuwa walio kuwa walinzi wa majengo mawili yaliyo haribiwa na ajali
hiyo nao ni majeruhi na wapo hospitali kwa matibabu. Benson Kibue ambaye ni mkuu
wa Polisi wa County ya Nairobi amesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi
alfajiri wakati ndege hiyo ya shirika la Skyward kuanguka na kuwaka moto.
Ajali hiyo ya ndege ya mizigo inayomilikiwa na shirika la Skyward, iliyokowa
ikisafirisha mzigo ilipata ajali muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa
Kimataifa wa Kenyataa mjini Nairobi iliyo kuwa ikisafirisha Mirungi kutoka
Kenya kuelekea Mogadishu, Somalia ndiyo iliyo chukua uhai wa raia wanne akiwemo
rubani mmoja na kujeruhi walinzi wawili huko mjini Nairobi.
0 comments:
Post a Comment