Muuguzi wa Hospitali ya Fortaleza Sao Paulo, Brazil aliyopelekwa Neymar baada ya kuumia wakati wa
mechi ya Brazil dhidi ya Colombia amefukuzwa kazi kwa kitendo chake cha kupiga
picha za video wakati akiwasili hapo na kuzirusha kwenye mitandao ya kijamii.
Picha hizo za video zilimwonyesha nyota huyo wa Brazil akipokelewa na
kukimbizwa kwenye varanda za hospitali hiyo na madaktari zilionekana muda mfupi
kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kutoka kwa taarifa kuwa Neymar hatoweza kucheza
mechi zote zilizobaki za Kombe la Dunia.
Muuguzi huyo alijulikana kwa sababu
mwisho wa video hiyo aligeuza kamera upande wake na kusema “woo-hoo!” na
kuonyesha tabasamu wakati nchi nzima ikiwa kwenye majonzi, pamoja na kushinda
2-1.
Kwa mujibu wa Globo, uongozi
wa hospitali umethibitisha kumfukuza muuguzi huyo kwa kitendo chake cha kuingilia
maisha binafsi ya mgonjwa, wakati huohuo; Fifa haitochukua hatua yoyote dhidi
ya beki wa Colombia aliyemuumiza Neymar, Fifa ilisema kamati ya nidhamu ilikaa
na “hakuna haja ya kuchukua hatua kwa tukio hilo’’ kwa sababu mwamuzi wa
mechi hakuona wakati Camilo Zuniga akimgonga na kuchukua uamuzi kwa wakati
0 comments:
Post a Comment