MKAZI wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma
Julietha Sokoine (24) ambaye amejifungua watoto wa watatu na ameiomba serikali,taasisi,mashirika na watu binafsi kumpatia msaada wa kifedha utakaomsaidia kuwatunza watoto hao.
Pia alisema msaada huo pia utamuwezesha kupata tiba ya ugonjwa wa pumu
ambao umemsababisha kuvimba mwili wote.
Akizungumza mwishoni mwa wiki, Sokoine ameiomba jamii kumsaidia kutokana na
kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu ambao pia umesababishia kuwa na
hali ngumu ya kimaisha ambayo inayomfanya kushindwa kuwatunza vizuri watoto
wake hao.
Alisema watoto hao, Daniel Sokoine,David Sokoine na Davis Sokoine
walizaliwa kwa pamoja Machi 22, mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa
Dodoma huku kati ya wawili wa wakiwa na uzito kilo mbili na nusu na wa
mwisho kilo mbili.
“Hali yangu siyo mzuri kutokana na mimi mwenyewe kukabiliwa na tatizo la
ugonjwa wa pumu,ambao pia wakati mwingine ninalazimika kuwanywesha maziwa
ya ngombe watoto hao pindi ninapozidiwa na ugonjwa huo”alisema .
Kwa upande wake baba wa watoto hao Sokoine Chipanta alisema pamoja na
juhudi nilizofanya za kilimo hata hivyo mazao yalinyauka na jua.
Alisema kutokana na hali hiyo analazimika kutafuta vibarua ili kuweza
kupata fedha kwa ajili ya kununua chakula pamoja na matunzo ya watoto hao.
Alisema kwa wale wote watakaoguswa na kuamua kumpa msaada wawasiliane naye
kwa namba ya simu 0652-744510.
0 comments:
Post a Comment