Monday, May 2, 2016

GETRUDE CLEMENT AREJEA: BUNGE LAMKARIBISHA


Getrude Clement mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza, leo amepata nafasi ya kufika bungeni Dodoma baada ya kupewa mwaliko wa Serikali 

Hivi karibuni Getrude  alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchiuliofanyika New York Marekani ambapo leo Bungeni  amewahimiza Watanzania kutunza mazingira na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.

Getrude amesema kuwa amefarijika kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana kusaini makubaliano ya Paris.

Katika kuwahimiza vijana kujenga tabia ya kutunza mazingira, Getrude amewaasa vijana hasa wanafunzi kusimamia suala la utunzaji wa mazingira wakiwa shuleni kwa kwa kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na klabu ya “Mali Hai” iliyopo shuleni anaposoma.

Kwa upande wa Watanzania kwa ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude amesema kuwa ni vema wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia utunzaji wa mazingira hasa matumizi ya mifuko ya plastiki.

Mwanafunzi huyo amekaribishwa na kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa heshima ya kuliwakilisha vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao na kusema “Ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana”.

Related Posts:

  • TASAF: MAJINA HEWA MRADI WA KUOKOA KAYA MASIKINI Wananchi wamemkataa mwenyekiti wa kitongoji cha Mwanogi kijiji cha Bulima, Kata ya Nyashimo wilayani Busega katika Mkoa wa Simiyu, wakimtuhumu kuweka majina hewa katika mradi wa kuokoa kaya masikini unaosimamiwa na Mfuko … Read More
  • TAKUKURU Kuchunguza Mabilioni ya Kikwete ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza kuchunguza fedha za uwezeshaji maarufu kama ‘Mabilioni ya JK’ ambazo hazikurejeshwa na wakopaji nchi nzima.  Msemaji wa Takukuru, Tunu Mleli alisema jan… Read More
  • MALI ZA PRINCE ZAHITAJI USIMAMIZI Nyota wa muziki wa Pop Prince hakuwacha wasia ,dadaake amefichua katika stakhabadhi za mahakama. Nakala zilizowasilishwa katika mahakama ya jimbo la Minnesota zinaonyesha,Tyka Nelson ametoa ombi la mtu atakayesimamia mal… Read More
  • Mkataba wa LugumiHii hapa ni taarifa ya Utekelezaji Ya Kamati Ndogo ya PAC Kuhusu Mkataba wa Lugumi … Read More
  • POLISI ABAKA MWANAFUNZI Mwanafunzi wa kidato cha tatu, juzi alimkaanga askari polisi anayedaiwa kumbaka kwa kuieleza Mahakama jinsi alivyotendewa kitendo hicho katika kibanda cha ulinzi cha benki. Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu wa Mahakama y… Read More

0 comments:

Post a Comment