Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen Kebwe ameamuru kukamatwa kwa Mwalimu Hamisi Salumu Mkoleme kwa tuhuma za kulipwa mishahara ya mwaka mmoja na nusu bila kufanya kazi katika kituo chake alichopangiwa baada ya uhamisho kutoka mkoa wa Tanga kwenda mkoa wa Morogoro bila kuripoti katika kituo alichopangiwa.
Akizungumza na walimu waliofika katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Mvomero ili kuhakikiwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro Dokta Kebwe Stephen Kebwe ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Mvomero kusimamia kwa ukamilifu zoezi hilo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wenyewe kutoa ushirikiano katika zoezi hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa amesema wameamua kuchukua hatua za kupitia upya orodha aliyokabidhiwa na Halmashauri ili kujiridhisha na kwamba iwapo itabainika mwalimu yeyote amefanya kosa kama hilo, hatua kali zitachukuliwa.
0 comments:
Post a Comment