Shirikisho
la soka Duniani FIFA limekatalia mbali ombi la rufaa la mchezaji wa Uruguay
Luis Suarez dhidi ya marufuku yake ya mizi minne kwa kosa la kumng'ata Mlinzi
wa Italia .
Katika
barua kwa wanahabari FIFA ilisema kuwa imekatialia mbali ombi la Shirikisho la
Soka la Uruguay la kuitaka kupunguza adhabu ya Mshambulizi huyo wa Liverpool .
Hata hivyo Suarez anauhuru wa
kukata rufaa katika mahakama ya rufaa ya michezo (Court of Arbitration for S port)
iwapo hataridhika na Uamuzi huo.
Mshambulizi huyo wa Liverpool
alibanduliwa nje ya kombe la dunia baada ya tukio hilo la Juni tarehe 24 na
sasa anaomba msamaha ili iwe rahisi kwake angalau kujifua pamoja na wachezaji
wenza huko Anfield Uingereza huku akitarajia uhamisho kuelekea Uhispania katika
klabu ya Barcelona .
Tukio hilo lilikuwa la tatu kwa mshambulizi huyo bora msimu
uliyopita huko Uingereza.
0 comments:
Post a Comment