Snura Mushi ni binti mwenye vipaji vingi ndani ya tasnia ya bongo movies. Pamoja na kuwa
mwigizaji aliyekuja kwa kasi sana pia Snura ni mwanamuziki wa bongo fleva
anayefanya vizuri sana sokoni kwa nyimbo zake mbalimbali zenye mahadhi ya pwani
mithili ya mduara. Pamoja na kuwa na umbo na sura nzuri ya kuvutia snura pia
amekuwa akitawala sana vichwa vingi vya habari,magazeti na redio kutokana na
uwezo wake mkubwa wa kukata kiuno kwenye nyimbo zake.
Snura Mushi (Jina lake halisi)
alizaliwa tarehe kumi na mbili (12) mwezi wa kwanza (1) mwaka 1984 Jijini Dar
es salaam ambako aliweza kukua na kupata elimu yake hapo hapo Dar es salaam.
Tofauti na
watu wengi wanavyofahamu,kipaji cha mwanadada Snura kilianzia kwenye
muziki kabla ya kuigiza na alikuwa na mwimbaji wa taarabu na kundi la “new best
star” mwaka 2004. Baada ya hapo alianzisha kundi lake la muziki aliloliita
“chanya na hasi” pamoja na vijana wawili mmojawapo akiwa marehemu sharo Milionea
kabla hajajiunga rasmi na sanaa ya maigizo. Kipaji cha mwanadada Snura
Kiligunduliwa na mtu aliyefahamika kwa jina la Siasa. Ambaye ndiye aliyemfuata
na kumshauri kuigiza baada ya kuvutiwa na uzuri na umbo lake ambalo kwa mujibu
wa mtu huyo alikuwa na “star look” na angeweza kufanya vizuri kama angejiingiza
katika sanaa. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2006. Na mwaka huo alipata nafasi ya
kuigiza kwenye Filamu ya Mfalme Seuta iliyodirectiwa na Gumbo Kihorota. Baadaye
aliweza kucheza movie za Zinduna na Hitimisho.
Snura alianza kujipatia umaarufu sana kupitia Filamu ya ITUNYAMA, na pia
kupitia igizo la Jumba la dhahabu alizofanya akiwa chini ya director Tuesday
Kihangala “Mr Chuzi”. Akizungumzia maisha yake ya ustaa, Snura anasema kuwa
huwa anaumizwa sana pale anapoona habari kwenye vyombo vya habari zinazomuhusu
ambazo mara nyingi anasema huwa si za kweli. Katika maisha yake ya kila siku
Snura hupendelea sana kukaa ndani na kutazama Filamu mbalimbali kwa ajili ya
kujifunza mambo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment