Wanawake wote walioamua kupamba
sehemu zao za siri kwa kuzitoboa wanachukuliwa kuwa wamepitia ukatili wa
kijinsia ama wamekeketwa kitengo cha afya kimetanabahisha hayo. Hata kama mtu
huyo amefikia umri wa utu uzima na ameyafanya hayo kwa ridhaa yake,bado
atahesabika kuwa alipitia ukatili wenye madhara kwa afya yake,na inapaswa
kuchukua tahadhari kubwa kuweka kumbu kumbu za watu walio toboa sehemu zao za
siri.
Lakini kujichora mwilini maarufu
kama Tattoo ama kutoboa sehemu za siri ama mwilini,kumepingwa na taasisi ya
utoboaji na uchoraji tattoo mwilini kwamba hakuna uhusiano wowote na ukeketaji.
Na kueleza kuwa vitu hivyo viwili havichangamani kulinganisha na kutoboa sehemu
za mwili wa mwanadamu,na taasisi hiyo wanachukulia suala la kutoboa mwili kama
jambo la kaiwada na la ridhaa anasema msemaji wa taasisi hiyo Marcus Henderson.
Zaidi ya matukio ya ukeketaji
yapatayo mia mbili yalichunguzwa na polisi wa kimataifa miaka mitano
iliyopita,na inashauriwa kama kuna mtu mmoja ana mashaka na suala ya ukeketaji
wataarifu polisi. Watoboaji makini huwa hawataki kuumiza wateja wao na huwa
hawataki kuonesha tundu za kazi zao na hawako tayari kumtoboa mtu aliye chini
ya umri wa miaka kumi na nane,anaeleza Mr Henderson.
Mtoboaji
maarufu amesema kwamba wateja wengi wanataka kutobolewa sehemu zao za siri
Mtoboaji maarufu kutoka mjini London
ambaye ametaka ahifadhiwe jina lake, amesema kwamba wateja walio wengi huwa
wanataka kutobolewa sehemu zao za siri zisilingane na ukeketaji.
Sihusiki na ukeketaji,nadhani
utoboaji ni zaidi ya pambo mwilini ama uvumbuzi mpya wa kihisia zaidi.
Mtoboaji huyu anadai kwamba huwa
anaitekeleza kazi yake kwa ufanisi mkubwa,kwanza huangalia picha kwa umakini
mkubwa kabla hajamtoboa mtu, na kamwe hawezi kumtoboa mtu aliye na umri wa
chini ya miaka kumi na nane.
Na wateja wake walio wengi ni
wanawake na hutoboa sehemu ya siri hasa kwenye pezi la sehemu ya kati ya maungo
ya mwanamke.
Ingawa mtoboaji huyu mashuhuri
mwanzoni alikuwa hakubali kutoboa sehemu za siri za wanawake,na hii ni kutokana
na maungo hao yalivyo na hatari inayowakabili kupitia utaratibu huo.
Naye msemaji kutoka kitengo cha afya
ambaye ni mwanamke anasema kwamba,kuna changamoto kwa baadhi ya maeneo wanawake
watu wazima hutobolewa sehemu zao za siri kilazima na maeneo mengine wasichana
hulazimishwa kutobolewa.
Wanawake waliotoboa sehemu zao za
siri watachukuliwa kuwa wamepitia ukatili ama wamekeketwa
Idadi ya wanawake waliokeketwa
nchini Uingereza inatajwa kufikia laki moja na elfu sabini,na zaidi ya wanawake
na wasichana elfu mbili na mia sita wamehudumiwa na kitabibu tangu September na
kati ya hao ,mia nne tisini na tisa walitambuliwa January mwaka huu pekee.
Nayo serikali ya Uingereza imesema
kwamba haina mpango wa kuifanyia marekebisho sheria ya mwaka 2003 kuingiza
suala la kufanya upasuaji kwa masuala ya urembo kwenye sehemu za siri.
Kamati teule ya wabunge katika
taarifa yake imesema kwamba sheria hiyo haina budi kubadilishwa ili kuweka wazi
juu ya taratibu hizo kuwa ni kinyume cha sheria na zaidi ni kosa la jinai kama
zitafanywa kwa msichana wa chini ya miaka kumi na nane isipokuwa kwa sababu ya
afya ya akili au kimwili.
abari kutoka BBC
0 comments:
Post a Comment