Tukio hilo lililotokea leo majira ya
2:35 asubuhi linadaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme katika jingo
hilo. Jengo la ‘Block B’ la Hostel za Mabibo, za wanafunzi wa
kike wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), jijini hapa limeungua kwa moto na kuteketeza
vifaa na mali kadhaa za wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye jengo hilo. Tukio
hilo lililotokea leo majira ya 2:35 asubuhi linadaiwa kusababishwa na hitilafu
ya umeme katika jingo hilo. Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza
Mukandala aliyekuwa eneo la tukio akiahidi kubeba dhamana ya kushughulikia
hasara ya mali, nyaraka na fedha kwa wanafunzi walioathiriwa na tukio hilo.
“Kwanza kuhusu vyeti vilivyoungua
,tutashughulikia vipatikane vyote.Pili tutashughulikia hata bajeti za kujikimu
kwa wale walioathirika, lakini pia kuanzia leo wanafunzi wote ambao walikuwa
kwenye jengo hilo watahamishiwa jengo lingine wakati huo uchunguzi ukifanyika
kufahamu chanzo cha moto,” alisema Profesa Mukandala. Kwa upande wake, Kamanda
wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alitoa tahadhari ya usalama kwa mali za
wanafunzi walioathiriwa na tukio hilo huku akisisiza utulivu wakati uchunguzi
wa chanzo hicho ukifanyika. Taarifa kutoka miongoni mwa wanafunzi hao
zimebainisha kuwa, wakati wa tukio hilo wanafunzi wawili wa kike waliruka
kutoka gorofa ya pili mpaka chini na kujeruhiwa vibaya.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) wakiangalia moja la bweni lililokuwa likiteketea leo katika
hostel za Mabibo.
|
Askari wa Zima Moto walifika eneo la
tukio hilo saa 3:45 asubuhi na kukuta moto ukiwa umeshapungua hatua
iliyosababisha wanafunzi hao kuwashambulia huku wakiwazomea na kuwataka
waondoke. Viongozi wawili wa zima Moto, Omary Katonga kutoka Ilala na Mboke
Msami wamesema changamoto kubwa iliyojitokeza ni kutopata taarifa mapema.
“Moto umetokea saa 2:35 asubuhi kwa
nini watujulishe tena kupitia Tanesco saa moja baadaye, tumefika hapa kwa
kutumia dakika 23, wanakosea kutulaumu ila kinachotakiwa ni taarifa mapema,”
amesema Katonga.
0 comments:
Post a Comment