Mbunge huyo alipanga kuliaga bunge
na alisema amekwishapata ruksa ya Spika kuwa angesimama bungeni kuwaaga wabunge
na wanachama wa Chadema baada ya chama hicho kumtimua uanachama wake hivi
karibuni, lakini ghafla mpango huo uliyeyuka kwa kile kilichoelezwa kuwa Spika
amemkatalia.
Tangu kuanzishwa kwa chama hicho
mwaka mmoja uliopita, Zitto amekuwa akihusishwa kukianzisha, hivyo kitendo
chake cha kujiunga nacho kitahitimisha mjadala wa muda mrefu wa mashabiki wake
waliokuwa wakihoji wapi ataelekea baada ya kung’olewa Chadema.
Akizungumza na gazeti hili jana,
Katibu Mkuu wa ACT, Samsom Mgamba aliangua kicheko na bila kuuma maneno
alisema: “Hahahaa... tutampokea kuanzia kesho (leo) na maandalizi
yamekamilika.”
Alipotakiwa kueleza wapi mapokezi
hayo yatafanyika alisema: “Hilo mbona liko wazi, yatafanyikia makoa makuu yetu
(yapo Makumbusho, Dar es Salaam) lakini kwa taarifa zaidi tutawajuza.”
Zitto anaingia ACT ikiwa ni siku
tisa kabla ya chama hicho kufanya uchaguzi wake mkuu, huku akitajwa kuwa
ameandaliwa kushika wadhifa wa mwenyekiti kuendeleza harakati zake za siasa.
Hivi karibuni, chama hicho kilimvua
uongozi aliyekuwa mwenyekiti mwanzilishi, Lucas Limbu kutokana na mgogoro
uliokuwapo baina ya viongozi na kufanya nafasi hiyo kubaki wazi.
Tayari washirika wa Zitto
waliohusishwa naye kuandika waraka wa mapinduzi ndani ya Chadema na baadaye
kufukuzwa uanachama, Mwigamba na Profesa Kitila Mkumbo wametua ndani ya chama
hicho kipya.
Chama hicho ambacho kinaendelea na
uchaguzi katika ngazi ya mikoa kikibakiza Mkoa wa Geita unaofanya uchaguzi wake
kesho. Kitaanza vikao vyake vya kitaifa Machi 27 na kuhitimisha kwa mkutano
mkuu Machi 29.
Akizungumzia uchaguzi huo, Mwigamba
alisema: “Maandalizi yanakwenda vizuri na hakuna shaka utafanikiwa kwa kiasi
kikubwa na tunawaomba Watanzania watuunge mkono.”
Tangu juzi, Zitto alitarajiwa
kuliaga Bunge lakini hakufanya hivyo kwa kilichoelezwa kuwa aliitwa na Spika wa
Bunge, Anne Makinda na kupewa ushauri kuwa afanye hivyo jana jioni.
Jana asubuhi mbunge huyo hakuingika
katika kikao cha Bunge lakini alionekana katika viwanja vya Bunge akiwa amevaa
shati la drafti na suruali ya kaki akizungumza na rafiki yake wa karibu, Deo
Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa kupitia CCM.
0 comments:
Post a Comment