Sunday, July 6, 2014

MEDEE AFUNGUKA NA UJIO WAKE MPYA


BAADA ya kupata maendeleo kutokana na kazi za muziki msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka kwenye kundi la Tip Top Connection Madee yupo katika maandalizi ya mwisho ya kuachia albamu yake ya pili ambayo ya kwanza ilitoka miaka 7 iliyopita.
Ambapo alionekana kusita kutoa albamu kwa kipindi hicho kutokana na kile wanachokiita mfumo mbovu wa usambazaji pamoja na mauzo ya albamu hiyo hali inayowapelekea baadhi ya wasanii kutoa vilio vya kupata hasara pindi wanapotoa albamu zao.
Baada ya kujikita kwenye maendeleo yanayotokana na kazi ya muziki, Madee amepanga kuachia albam yake mpya October mwaka huu ikiwa ni albam ya kwanza kutoka kwake tangu aachie albam yake ya mwisho miaka saba ilioyopita.
Akizungumza jijini Hi5 Media, Madee amesema kuwa hivi sasa anaona umuhimu wa kutoa albam kwa sababu ameona licha kutopata fedha za kutosha kwenye biashara hiyo, kuacha kutoa albam ni kama kumnyima haki shabiki wake.
“Mimi mwenyewe zaidi nina mangoma kama 50 ambayo haujayasikia yako tu ndani hayana mpango wowote. Lakini unafikiria utatoa albam utapata nini. Lakini pia unakuta unamzulumu yule shabiki wako ambaye yuko mbali anataka kusikiliza ngoma za Madee, anataka kushika albam ya Madee. Lakini anakuwa hapati kwa sababu umesitisha kutoa albam.” Amesema Madee.
Amesema hata msanii anapoenda katika bara la Ulaya kutangaza muziki wake haulizwi idadi ya nyimbo alizotoa bali idadi ya albam alizotoa.

0 comments:

Post a Comment