Mwanamume mmoja nchini Saudia amempa
talaka mkewe kutokana na ujumbe wake katika mtandao wa WhatsApp. Kulingana na
gazeti moja la kiharibu Al Hayat, mwanamume huyo amedai kwamba mkewe aliandika
ujumbe unaosema ''naomba kuwa na subra ya kutosha ili kuweza kuishi na wewe''.
''Nilimpigia mmoja ya ndugu zangu
kumuuliza iwapo ujumbe ule ulikuwa unanilenga mimi'', alisema mwanamume
huyo.Watu wa Familia yangu walithibitisha hilo na nilisikia aibu kubwa kwamba
mabibi za marafiki zangu pamoja na watu wa familia yangu wanaona
ninaaibishwa.Hata sielewi alikuwa akimaanisha nini''.Amesema kuwa ndo yake
ilikuwa taabani na kwamba kitendo hicho hakikustahili kufanyika.Si mara ya
kwanza amenichafulia jina katika mtandao wa kijamii.Niliamua kumpa talaka kabla
ya kuyatamgaza maisha yangu katika mitandao ya kijamii.'',
Khalid Al Habibi ,naibu mkurugenzi
wa kituo cha kijamii kinachojihusisha na watoto mayatima anasema kuwa mitandao
ya kijamii ni chanzo kikuu cha talaka.
0 comments:
Post a Comment