Klabu ya Liverpool imemsajili rasmi
mshambuliaji machachari Mario Balotelli kwa jumla ya kiasi cha paundi milioni
16. Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa wameamua kumchukua
mshambuliaji huyo ili kuziba pengo lililoachwa wazi na Luis Suarez ambaye
amehamia Barcelona. Balotelli ambaye mwaka jana alijiunga na timu ya AC millan
kwa uhamisho wa paund milion 19 akitokea Machester City hadi sasa ameweza
kufunga magoli 30 katika michezo 54. Balotelli alijiunga na Manchester City
August 2010 kwa paundi milion 24 wakati huo akitokea Inter Milan ambako
aliiwezesha klabu yake kuchukua kombe katika michuano ya ligiya England.
0 comments:
Post a Comment