Moto wateketeza afisi za NFF Abuja
Moto mkubwa umetekeza makao ya shirikisho la soka la Nigeria
NFF iliyoko Abuja, moto uliowachukua zaidi ya saa mbili kuuzima huku
wakisaidiana na umma kuuzima moto huo mkubwa . Afisa wa kuzima moto Eyo amesema
kuwa wanashuku ya kwamba chanzo cha moto huo ulitokana na hitilafu ya umeme.
Katibu mkuu wa NFF bwana Musa Amadu amesema kuwa moto huo ulianzia katika
afisi ya mhasibu wa shirikisho hilo."Niliwasili kama kawaida lakini nikakatazwa kupanda ghorofa kwani tayari moshi ulikuwa unafuka ''
"Wafanyikazi wa shirikisho hilo wangeweza kuzima moto huo lakini walishindwa kuingia ofisini humo na hivyo hawangfeweza kubaini chanzo kikamilifu''
''Hata hivyo nashukuru mungu kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha yake kutokana na moto huo kwahivyo hakuna faida ya kumlaumu mtu yeyote''
Mwenyekiti wa NFF Aminu Maigari anakumbwa na tuhuma za
uongozi duni kutokana na mkasa huo wa moto ni pigo kwa shirikisho hilo ambalo
tayari linakabiliwa na mvutano wa uongozi ambao umepelekea kung'olewa
madarakani kwa mwenyekiti Aminu Maigari mara mbili akirejeshwa
0 comments:
Post a Comment