Thursday, March 26, 2015

NDEGE ILIYO ANGUKA UFARANSA, ILIANGUSHWA MAKUSUDI



Rubani wa ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya jumanne alitaka kuiharibu ndege hiyo kulingana na maafisa wa Ufaransa.Kiongozi wa mashtaka katika mji wa Mersaille ,Brice Robin, akizungumza kulingana na habari aliyopata katika kijisanduku cha kunasa sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa ndani ya chumba cha kuendesha ndege pekee.


Rubani huyo kimakusudi aliishusha ndege hiyo kwa kasi huku rubani mwenza akiwa nje ya chumba hicho cha kuendesha ndege.
Bwana Robin amesema kuwa kulikuwa na kimya kikubwa ndani ya chumba hicho wakati rubani mwenza alipojaribu kuingia kwa nguvu.
Hatahivyo abiria walisikika wakipiga nduru kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo,aliongezea.
 
Rubani huyo kwa jina Andreas Lubtiz,mwenye umri wa miaka 28, alikuwa hai hadi wakati ndege hiyo ilipoanguka ,kiongozi wa mashtaka alisema.


Ndege hiyo aina ya Airbus 320 iliokuwa ikitoka Barcelona kuelekea Duesseldorf Ujerumani iligonga mlima na kuwauwa abiria wote 144 pamoja na wafanyikazi sita wa ndege baada ya kushuka kwa dakika nane.
"Tunasikia rubani akimuuliza rubani mwenza kuchukua udhibiti wa usukani wa ndege hiyo na vilevile tunasikia sauti ya kiti kikisonga nyuma na mlio wa mlango ukifungwa,bwana Robin aliwaeleza wanahabari.

Related Posts:

  • MALI ZA PRINCE ZAHITAJI USIMAMIZI Nyota wa muziki wa Pop Prince hakuwacha wasia ,dadaake amefichua katika stakhabadhi za mahakama. Nakala zilizowasilishwa katika mahakama ya jimbo la Minnesota zinaonyesha,Tyka Nelson ametoa ombi la mtu atakayesimamia mal… Read More
  • 3,551 WASAMEHEWA Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,551, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Muungano wa Tanzania. Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projest Rwegas… Read More
  • POLISI ABAKA MWANAFUNZI Mwanafunzi wa kidato cha tatu, juzi alimkaanga askari polisi anayedaiwa kumbaka kwa kuieleza Mahakama jinsi alivyotendewa kitendo hicho katika kibanda cha ulinzi cha benki. Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu wa Mahakama y… Read More
  • TASAF: MAJINA HEWA MRADI WA KUOKOA KAYA MASIKINI Wananchi wamemkataa mwenyekiti wa kitongoji cha Mwanogi kijiji cha Bulima, Kata ya Nyashimo wilayani Busega katika Mkoa wa Simiyu, wakimtuhumu kuweka majina hewa katika mradi wa kuokoa kaya masikini unaosimamiwa na Mfuko … Read More
  • RUSHWA:OFISA WA TRA KIZIMBANI Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Amani Mkwizu na mfanyakazi wa kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, Edward Magobela wamepandishwa kortini jana wakikabiliwa na mashtaka matatu ya rushwa.  Washtakiwa ha… Read More

0 comments:

Post a Comment