Rais Kenyatta aliwataka maafisa wote
wa umma waliotajwa katika ripoti hiyo waondoke ilituhuma zote dhidi yao
zichunguzwe kwa kina na tume ya kupambana na ufisadi.
''Kwa hakika imewadia wakati ambapo
serikali yangu haina budi ila kuchukua hatua mahsusi ambayo inalenga kukomesha
hili zimwi la ufisadi mara moja''
UFISADI ''Ufisadi umevuka mipaka na lazima nasi tujifunge kibwebwe
na kukabiliana nao''.
''Natarajia kuwa wale waliotajwa
katika ripoti hii watanga'tuka mamlakani hadi pale uchunguzi utakapokamilishwa
ndipo warejee afisini.'' alisema Kenyatta.
Kenyatta aliongezea kusema kuwa
''Ninamtaka kiongozi wa mashtaka ya umma kuanzisha uchunguzi mara moja
kuhusiana visa vyote vilivyotajwa humu katika kipindi cha siku 60 zijazo''.
Ripoti hiyo iliyotayarishwa na tume
ya kupambana na ufisadi nchini Kenya KACC inawadia wakati ambao kumekuwa na
visa vingi vya ufisadi haswa katika serikali kuu na pia serikali za majimbo.
Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu
ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Kisa kilichozua mjadala ni kile cha
'Anglo Leasing'' ambayo ilijumuisha kandarasi za idara ya Uhamiaji idara ya
upelelezi na Idara ya usalama wa taifa.
Mabilioni ya fedha yalilipwa kwa
wanakandarasi waliotarajiwa kuwasilisha kazi ambazo hazikuwahi kufanyika hata
wa leo.
Magavana 10 kati ya 47 wametajwa
katika ripoti hiyo ambayo itatangwwa rasmi siku ya jumanne katika mabunge yote
mawili.
Duru zinasema kuwa Kamati nzima ya
bunge inayochunguza ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma imetajwa katika
ripoti hiyo.
MSAMAHA
Aidha Rais Kenyatta aliwaomba radhi
maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Kenyatta alisema''ili wakenya waweze
kusonga mbele na kusahau yaliyopita kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali
zilizotangulia ni wajibu wangu
kuchukua fursa hii na kuwaomba
msamaha wote waliodhulumiwa kwa njia moja au nyengine.
Zaidi ya Wakenya 650,000 walifukuzwa makwao kufuatia vita vya baada ya
uchaguzi wa mwaka wa 2008 na tume maalum ya haki ukweli na maridhiano TJRCilipendekeza kuwa sharti serikali iombe radhi kwani fedha haziwezi kufuta machungu ya mateso ambayo wakenya wamepitia''
''Hata hivyo licha ya mapendekezo ya tume hiyo ya maridhiano,nimeagiza wizara ya fedha itenge shilingi bilioni 10 dola milioni 110, katika kipindi cha miaka
mitatu ijayo kwa ajili ya kuwafidia wale wote walioathirika''
0 comments:
Post a Comment