Ohoo, ama kweli dunia imekwisha! Mtumishi wa Mungu (Muinjilisti) ambaye
kipindi chake cha dini kinarushwa katika kituo kimoja maarufu cha
televisheni Bongo (Jina tunalihifadhi) aliyefahamika kwa jina la
Fredrick Kishindo ‘Badoo’ hivi karibuni alipata aibu ya kufungulia mwaka
2015 baada ya kunaswa na mke wa mtu chumbani, Risasi lina mkanda nzima.
Mtumishi Fredrick Kishindo ‘Badoo’ Akijitete
Ilikuwaje?
Awali chanzo cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa,
Januari 11, mwaka huu Muinjilisti huyo anayesifika kwa kuhubiri watu
waache dhambi alionekana akinyata kuingia kwenye nyumba ya mke wa mtu
huyo iliyopo Sinza jijini Dar huku kukiwa na taarifa kuwa, mume wa
mwanamke huyo alikuwa safarini.
Wifi mtu atonywa
Ikaelezwa kuwa, kufuatia mazingira hayo wifi wa mwanamke huyo alitonywa
juu ya taarifa za Badoo kuingia kwenye nyumba ya kaka yake, maelezo
yaliyomshitua hivyo kulazimika kuelekea eneo la tukio.
Baada ya wifi mtu huyo kufika nyumbani kwa kaka yake na kuhakikishiwa
kuwa Badoo yuko ndani, aliuliza namna ya kuwapata makamanda wa
Operesheni Fichua Maovu ya Global Publishers ‘OFM’ ambapo mmoja wa
majirani alimpatia namba ya simu, akawapigia.
Polisi washirikishwa
Katika kuhakikisha usalama katika eneo hilo, wifi huyo pia
aliwasimamisha polisi waliokuwa doria na kuwatonya juu ya uzinzi
unaofanyika nyumbani kwa kaka yake na kwa kuwa kazi ya askari ni kulinda
raia na mali zao, walitoa ushirikiano.
OFM watinga eneo la tukio
Baada ya makamanda wa OFM kupigiwa simu na kunyetishiwa juu ya uwepo wa
Muinjilisti huyo chumbani na mke wa mtu, kwa kutumia pikipiki zao
ziendazo kasi walianza safari na baada ya dakika chache walikuwa
wamefika kwenye nyumba hiyo na kuwakuta polisi.
Muinjilisti, mke wa mtu live
Polisi wakiwa na OFM waliongozwa na wifi mtu huyo hadi kwenye chumba
ambacho madhambi yalikuwa yakitendeka, walipoingia walikuta mke wa mtu
na mtumishi huyo wa Mungu wakiwa kama walivyozaliwa.
Aibu iliyoje!
Baada ya kuona ‘picha imeungua’, mtumishi huyo alisikika akisema kuwa
amepata aibu ambayo hakuitarajia huku akiomba asipigwe picha wala
kufanyiwa kitendo kibaya bali apewe nafasi ya kujitetea.
Aidha mke wa mtu aliyenaswa akimsaliti mumewe alionekana kutahayari na
aliishiwa nguvu zaidi alipomuona wifi yake aliyekuwa amefura ile mbaya.
Utetezi wa mtumishi wa Mungu
Kufuatia kunaswa huko, Badoo alijitetea kwa kujichanganya, awali alisema
aliitwa na mwanamke huyo kwa ajili ya kuongea mambo ya biashara na
kwamba eti walivua nguo kutokana na hali ya joto iliyokwemo chumbani
humo.
Kana kwamba alihisi kajichanganya, Muinjilisti huyo aligeuza utetezi na
kusema aliingia majaribuni baada ya kushawishiwa na ibilisi kisha
mwanamke huyo hakumwambia kuwa ana mume.
Bofya hapa usikie utetezi wake
“Jamani naomba mnisamehe, si kosa langu bali ibilisi ndiye
aliyenishawishi na huyu mwanamke hakuniambia kama ana mume. Hapa
aliniita kwa ajili ya biashara flani.
“OFM nawajueni lakini niko chini ya miguu yenu, naomba msiitoe habari
hii gazetini kesho n’tawaletea chochote pale ofisini kwenu, si ni pale
Bamaga ee, napajua sana pale”.
OFM ni mwiko kupokea rushwa
Licha ya utetezi wake huo, makamanda wa OFM walisimamia weledi wa kazi
yao na kumweleza kuwa, rushwa kwao ni mwiko hivyo kama atafika ofisini
kwao iwe ni kwa ajili ya maelezo zaidi ya kwa nini amevunja moja ya amri
kumi za Mungu.
Mpaka OFM wanaondoka eneo la tukio, mke wa mtu huyo alikuwa akiendelea
kumuomba msamaha wifi yake huku Muinjilisti naye akijaribu kutuliza
mambo yasifike mbali akidai kuwa, mke wake, ndugu na marafiki wakijua
ataaibika.
Chanzo:Global Publishers