Thursday, July 10, 2014

WANNE WAUWAWA KATIKA AJALI YA NDEGE NAIROBI

WAWILI KUWAHISHWA HOSPITALI WAKIWA MAJERUHI


Watu wanne wameripotiwa kuuwawa asubuhi ya Jumatano baada ya ndege ya mizigo kuanguka katika mtaa wa Utawala mjini Nairobi na kusababisha uharibifu wa majengo mawilli kabla ya ndege hiyo kuanza kuwaka moto
Mbali na ndege hiyo kusababisha vifo vya watu wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo akiwemo na rubani aliye kuwa akipaisha ndege hiyo chanzo cha habari kinaeleza kuwa walio kuwa walinzi wa majengo mawili yaliyo haribiwa na ajali hiyo nao ni majeruhi na wapo hospitali kwa matibabu. Benson Kibue ambaye ni mkuu wa Polisi wa County ya Nairobi amesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi alfajiri wakati ndege hiyo ya shirika la Skyward kuanguka na kuwaka moto.
Ajali hiyo ya ndege ya mizigo inayomilikiwa na shirika la Skyward, iliyokowa ikisafirisha mzigo ilipata ajali muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa Kimataifa wa Kenyataa mjini Nairobi iliyo kuwa ikisafirisha Mirungi kutoka Kenya kuelekea Mogadishu, Somalia ndiyo iliyo chukua uhai wa raia wanne akiwemo rubani mmoja na kujeruhi walinzi wawili huko mjini Nairobi.

0 comments:

Post a Comment