• This is Slide 1 Title

    This is slide 1 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 2 Title

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 3 Title

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday, December 20, 2014

MOJA KATI YA DEMONSTATION ZA VISUALIZED EFX


Thursday, November 13, 2014

Blog Hi5: JXJ AKIFANYA YAKE KATIKA JUKWAA LA KONGWA AFRIKA P...

Blog Hi5: JXJ AKIFANYA YAKE KATIKA JUKWAA LA KONGWA AFRIKA P...: Moja kati masaani wa Muziki wa Kizazi kipya anayefanya vizuri katika kazi zake ambaye yuko chini ya lebo ya DomTown Records JX, hapo akiwa...

JXJ AKIFANYA YAKE KATIKA JUKWAA LA KONGWA AFRIKA PAMOJA PROJECT

Moja kati masaani wa Muziki wa Kizazi kipya anayefanya vizuri katika kazi zake ambaye yuko chini ya lebo ya DomTown Records JX, hapo akiwa anafanya yake katika show iliyo andaliwa na kampuni ya Akonshaz Music ndani ya kitengo cha Muziki chini ya project ya Afrka Pamoja

DENI LA BILIONI 102 MSD: SERIKALI YAWEKWA KITIMOTO BUNGENI

MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, mkoani Rukwa, Bw. Ally Mohamed Kessy (CCM), ameitaka Serikali itoe tamko la haraka kuhusu hali ya upatikanaji huduma za afya katika hospitali za umma.
Alisema hivi sasa maafa yanayowapata Watanzania kutokana na uhaba wa dawa katika hospitali na vituo vya afya vilivyopo chini ya Serikali ni zaidi ya vifo vilivyotokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea nchini Rwanda na Burundi.
Bw. Kessy aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana baadaya kuomba mwongozo na kusisitiza kuwa, hali ya upatikanaji dawa katika hospitali na vituo vya afya ni mbaya.
“Madhara yanayotokana na ukosefu wa dawa ni zaidi ya vita vilivyotokea Rwanda na Burundi... naiomba Serikali iache mzaha na suala hili, itoe tamko haraka ili Watanzania wajue la kufanya,” alisema Bw. Kessy.
Siku chache zilizopita, Mbunge wa Kisesa, mkoani Simiyu, Bw. Luhaga Mpina, alilitaka Bunge kusitisha vikao vyake ili fedha zinazotumika kuwalipa posho, zitumike kulipa deni ambalo Serikali inadaiwa na Bohari ya Dawa (MSD).
Deni hilo ni sh. bilioni 102 hali inayosababisha MSD ishindwe kumudu gharama za kuagiza dawa nje ya nchi.
Akisisitiza msingi wa hoja yake, Bw. Kessy alisema kutokana na tatizo hilo, Watanzania wengi wanapoteza maisha hasa watoto na wajawazito; hivyo ni vyema Serikali ikatoa tamko la kupatikana ufumbuzi wa tatizo hilo haraka iwezekanavyo.
Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya, alisema mashine ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi katika Hospitali ya Ocean Road, ni mbovu isipokuwa moja ambayo nayo inafanya kazi kwa kusuasua hali ambayo inasababisha mateso makubwa kwa wagonjwa wanawake.
“Hadi sasa, hali ya huduma za afya pale Ocean Road ni tete, mashine ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi imekufa, inayofanya kazi ni moja tena kwa kusuasua...Serikali itoe tamko ili kunusuru maisha ya wanawake, hali ni mbaya,” alisema.
Akitoa ufafanuzi wa suala hilo kwa niaba ya Serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandyosa, alisema suala la tiba ni muhimu kwa uhai wa binadamu ambapo Serikali inatambua tatizo lililopo.
Alisema Serikali itatoa tamko rasmi bungeni hivyo aliwaomba wabunge kuwa na subira ambapo Prof. Mwandosya, pia alitolea ufafanuzi kuhusu mwongozi ulioombwa na Mbunge wa Mbozi Magharibi, mkoani Mbeya, Bw. David Silinde (CHADEMA).
Katika mwongozo huo, Bw. Silinde alitaka Serikali itoe tamko kuhusu madeni ya wakulima wa mahindi waliyouza kwa Wakala wa Hifadhi ya Taifa (NFRA), yaliyodumu kwa miezi mitatu lakini Serikali imekaa kimya bila kutoa kauli yoyote.
Bw. Silinde alisema wakulima hao wamelima mahindi na sasa hawanufaiki nayo kwani mbali na kuendelea kuidai Serikali, mengine yanaoza kwa kukosa soko na kuwasasabishia umaskini.
Akijibu hoja hiyo, Prof. Mwandosya alisema ni kweli suala la wakulima wa mahindi limezungumza sana ambapo Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, itatoa tamko la Serikali wiki hii.

Bunge hilo liliendelea kujadili mpango wa maendeleo ambapo Mbunge wa Mbeya Mjini, Bw. Joseph Mbilinyi (CHADEMA), alidai kusikitishwa na kauli aliyoiita nyepesi.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe kuhusu kuenea kwa habari za Rais wa China kuondoka na meno ya tembo alipokuja nchini.
Alisema Bw. Membe alitoa kauli nyepesi ambayo kila akiitafakari anashindwa kuelewa hasa ukizingatia suala hilo ni nyeti na linagusa masilahi ya Taifa; hivyo alistahili kulieza Bunge kwa umakini si kama alivyofanya.
“Nimesikitishwa na kauli ya Waziri Membe, nilitegemea kuona akiliambia Bunge hatua zilizochukuliwa na Serikali au kuunda tume ili iweze kubaini ukweli wa jambo hilo badala ya kutoa taarifa za kukanusha bungeni.
“Mbali ya Rais wa China kuchafuliwa, Taifa letu pia limechafuka kwa sababu suala hili limezungumzwa katika vyombo vya habari ambavyo vingi ni vya kimataifa,” alisema.

Monday, November 10, 2014

Hi5 Afya Leo EP 1_Vidonda Vya Tumbo

Tuesday, November 4, 2014

Crown Jay AKIZUNGUMZIA NGOMA YAKE MPYA

Msani anaye julikana kwa jina la Crown Jay mkali wa miondoko ya style za akina MikMill, Crunk Master wa DomTown hivi karibuni amefanya interview na Hi5 Media akizungumzia juu ya project yake mpya inayo kuja ambayo bado ipo jikoni ikipikwa ili kuhakikisha inakuja kufanya vizuri katika soko la muziki wake.

Wednesday, October 22, 2014

TAFAKARI

Tafakari...!

TANZANIA KUPATA NEMBO YAKE YA BIASHARA



MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tan Trade), ipo katika mchakato wa kuandaa nembo ya kibiashara itakayoitambulisha na kuitangaza Tanzania katika suala zima la uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika mkutano wa mchakato wa kupata usajili wa kuwa na nembo mpya ya Taifa, Mkurugenzi wa Tan Trade, Jacqueline Maleko, alisema kuwa ni vema ifikapo mwakani wakapata usajili  utakaosaidia taifa kuwa na nembo  yake.
Alisema endapo watafanikiwa kupata usajili Tanzania itatangazika katika uwekezaji na kwamba hakuna nchi itakayoweza kujitambulisha kibiashara kwa kutumia rasilimali za taifa.
Maleko aliongeza kuwa  Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo pia ni adimu kupatikana katika nchi  nyingine yeyote duniani na kwamba baadhi ya nchi zikifanya upotoshaji wa makusudi na  kujitangaza kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini.
Aliongeza kuwa  licha ya  mchakato kuwa na changamoto zake kwa kuhitaji  fedha nyingi mamlaka yake itahakikisha  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanafanikisha suala hilo alilolitaja kuwa ni  kilio chao cha muda mrefu.
Maleko alisema katika kuhakikisha wanafanikiwa katika azma hiyo ya kupata nembo ya Taifa ya kibiashara mamlaka yake itashirikiana na  kampuni ya Squire Patton Boggs kutoka nchini Marekani.
Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama   wa Tanzania  (TPSF),  Geofrey Simbeye alisema nchi imechelewa  kupata nembo ya  taifa na kwamba suala hilo lilipaswa kufanywa miaka 10 iliyopita na kuwataka wadau kuhakikisha suala hilo

MADEREVA, MAKONDAKTA UDA KUKIONA



ABIRIA wa mabasi jijini Dar es Salaam, wameshauriwa kusaidia kudhibiti uendeshaji holela na tabia zisizokubalika zinazofanywa na baadhi ya madereva na makondakta kwa kupiga simu zilizochapishwa katika mabasi yote ya Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA).
Taarifa ya UDA iliyotolewa jijini Da es Salaam jana na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, George Maziku, ilieleza kuwa utumiaji wa namba hizo utaisaidia pia kampuni kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja wake.
“Tunawakumbusha wateja wetu pamoja na watumiaji wengine wa barabara kuripoti uzembe wowote au utovu wa nidhamu utakaofanywa na madereva na makondakta wa UDA, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
“Mbali na kuboresha utoaji wa huduma zetu, UDA inalenga kuwa mfano wa kuigwa kwa mabasi mengine ya abiria nchini katika uzingatiaji wa sheria, utoaji wa huduma nzuri kwa wateja na kuwa kichocheo cha kupunguza foleni katikati ya jiji la Dar es Salaam,” alisema.
Maziku alisema uongozi wa UDA utachukulia kwa uzito mkubwa na kuyafanyia kazi maoni yote yakayokuwa yakitolewa kupitia namba hizo, ili kuondokana na dhana potofu kwamba wamiliki na waendeshaji wa kampuni za magari ya abiria ni watu ambao hawajaelimika.
Alisema  mbali na uwepo wa namba hizo za simu, UDA itaendelea na utekelezaji wa utaratibu wake wa kutuma waratibu kupanda mabasi ya kampuni hiyo na kuripoti juu ya utendaji kazi wa madereva na makondakta wa mabasi hayo.


Tuesday, October 21, 2014

DIAMOND ANASWA AKIWA KITANDANI NA WEMA

Wema sepetu akilalamika juu ya jokate kipande hiki kina sauti ya wema akiwa anatoa ya moyoni kwa Jocate

NEW OFFICIAL VIDEO LIL WYNE_KRAYZ

Wanamuaita walking mesiums kwa alivyo chafukwa na Tattoo za kutosha zenye kumbukumbu tofauti tofauti kulingana na aliyokwisha pitia

DIAMOND PLATNUM SERENGETI FIESTA FULL SHOW

Anayepeta kwa Ubunifu na umahiri katika tungo zake za nyimbo mbalimbali ambaye kwa sasa anamekuwa nominated kunyang'anyia tuzo ya msanii bora wa Afrika pamoja na East Africa ndani ya MTV akiwa katika safu moja na mtu mzima Davido wa Nigeria. Tuamke watanzania na kumpigia kura msanii wetu aweze kuiwakilisha Tanzania vyema huko kunako MTV.

SERENGETI FIESTA 2014 TANGA_ALI KIBA

Huyu ndiye mflame ambaye kiti chake hakina mrithi akifanya show ya serengeti fiesta Tanga 2014

Monday, October 13, 2014

Hi5: NEW BONGO MUVIE NA UJIO WA VISUALIZED EFX

NEW BONGO MUVIE NA UJIO WA VISUALIZED EFX


Kutoka Visualized EFX, siku chache zilizopita walikuwa location wakifanya mazoezi ya kushuti falamu mpya inayohusu maisha ya kijana aliye rithishwa uchawi kimakosa kulingana na jinsi anavyo utumia katika mazingira anayoishi. Bloger wetu alipata nafasi ya kwenda kushuhudia zoezi hilo na pia aliongea na uongozi ambao haukuwa tayari kuzungumza chochote juu ya filamu hiyo kwa kuwa ndio kwanza ipo katika maandalizi na kusema chochote  itakuwa mapema kuwajulisha wadau wa VEFX. Pia waliongezea kwa kusema wanahita kufanya vitu tofauti na ndio maana wanachukua muda mrefu kuandaa kazi zao mbali na hilo uchache wa vifaa wanavyo hitaji kufanyia kazi. 


Moja kati ya assistance director pia ndiye mtunzi filamu za Visualized EFX Mr. Jackson a.k.a Jackcty alizungumza machache kuhusu kazi zinazo kuja mbeleni kuwa kuna kipindi kinafanyiwa final editing then soon kitakuwa kwa mtandao pia wadau wafahamu ya kuwa kampuni haina kazi moja tu ya kuandaa filamu ni pamoja kushuti vipindi, matangazo ya pamoja na event mbalimbali kwahiyo  wadau wajiandae kupokea mengi kutoka VEFX.


“Tasnia ya Bongo movie ina changamoto nyingi kama Visualized EFX tunaandaa wasanii ambao watakuwa chini ya kampuni ya VEFX ambayo ni tawi la Akonshaz Music Co, na mara nyingi tunapenda kuandaa kazi zetu kwa wasanii ambao wako na malengo na ndio maana mpaka sasa ziko demo tu ambazo hivi karibuni mtazipata katika chombo cha habari cha Hi5 Media”hayo yalikuwa ni maneno yake mkuu wa kitengo kutaka Visualized EFX.

Thursday, September 11, 2014

NONDO Ep1: Ben Carson Biograph



Ben Carson Biography
Surgeon, Philanthropist, Journalist (1951–)
Ben Carson overcame his troubled youth in inner-city Detroit to become a gifted neurosurgeon famous for his work separating conjoined twins.
Ben Carson was born in Detroit, Michigan, on September 18, 1951. His mother, though undereducated herself, pushed her sons to read and to believe in themselves. Carson went from being a poor student to receiving honors and he eventually attended medical school. As a doctor, he became the Director of Pediatric Neurosurgery at Johns Hopkins Hospital at age 33, and became famous for his ground-breaking work separating conjoined twins.

Early Life

Benjamin Solomon Carson was born in Detroit, Michigan, on September 18, 1951. The second son of Sonya and Robert Solomon Carson, Ben grew up in the hardened climate of inner-city Detroit. Ben's mother was raised in Tennessee in a very large family. She dropped out of school in the third grade.
With not much hope or prospects in life, she married Baptist minister Robert Carson when she was 13, believing that he would change her life. The couple moved to Detroit, Michigan, and for a time, the marriage was a success. Carson showered his wife with gifts and attention. But over time, Robert Carson changed. Though benevolent, he could also be domineering and erratic. In time, Sonya felt it was best for her sons if she and Robert divorced.

Influential Mother

Ben was 8 and Curtis, Ben's brother, was 10 when Sonya was left to raise the children on her own. The family was very poor, and to make ends meet Sonya sometimes took on two or three jobs at a time in order to provide for her boys. Most of the jobs she had were as a domestic servant. There were occasions when her boys wouldn't see her for days at a time, because she would go to work at 5:00 a.m. and come home around 11:00 p.m., going from one job to the next.
Carson's mother was frugal with the family's finances, cleaning and patching clothes from the Goodwill in order to dress the boys. The family would also go to local farmers and offer to pick corn or other vegetables in exchange for a portion of the yield. She would then can the produce for the kids' meals. Her actions, and the way she managed the family, proved to be a tremendous influence on Ben and Curtis.
Sonya also taught her boys that anything was possible. By his recollection many years later, Ben Carson had thoughts of a career in medicine, though it was more of a fantasy many young children harbor as they grow up. Because his family was on medical assistance, they would have to wait for hours to be seen by one of the interns at the hospital. Ben would listen to the pulse of the hospital as doctors and nurses went about their routines.
Occasionally, there'd be an emergency and he could hear in people's voices and in their quick movements the pace and emotions rise to meet the challenge. He'd hear the PA system call for a "Dr. Jones" and fantasized that one day they'd be calling for a "Dr. Carson."

Early Education

Both Ben and his brother experienced difficulty in school. Ben fell to the bottom of his class, and became the object of ridicule by his classmates. He developed a violent and uncontrollable temper, and was known to attack other children at the slightest provocation. The poverty he lived in and the difficult times he experienced in school seem to exacerbate the anger and rage.
Determined to turn her sons around, Sonya limited their TV time to just a few select programs and refused to let them go outside to play until they'd finished their homework. She was criticized for this by her friends, who said her boys would grow up to hate her. But she was determined that her sons would have greater opportunities than she did.
She required them to read two library books a week and give her written reports, even though with her poor education, she could barely read them. She would take the papers and pretend to carefully review them, scanning over the words and turning the pages, before placing a checkmark at the top of the page to show her approval.
At first, Ben resented the strict regimen. While his friends were playing outside, he was stuck in the house, forced to read a book or do his homework. But after several weeks of his mother's unrelenting position, he began to find enjoyment in reading. Being poor, there wasn't much opportunity to go anywhere. But between the covers of a book he could go anyplace, be anybody and do anything.
Ben began to learn how to use his imagination and found it more enjoyable than watching television. This attraction to reading soon led to a strong desire to learn more. Carson read books on all types of subjects and found connections between them. He saw himself as the central character of what he was reading, even if it was a technical book or an encyclopedia. He read about people in laboratories, pouring chemicals into a beaker or flask, or discovering galaxies, or peering into a microscope.
He began to see himself differently, different than the other kids in his neighborhood who only wanted to get out of school, get some nice clothes, and a nice car. He saw that he could become the scientist or physician he had dreamed about. Staying focused on this vision of his future helped him get through some of the more difficult times.
Within a year, Ben Carson was amazing his teachers and classmates with his improvement. The childrens' books he read while he was confined to quarters now had relevancy in school. He was able to recall facts and examples from the books and relate them to what he was learning in school. In 5th grade, Ben astonished everyone by identifying rock samples his teacher had brought to school.
As he recalled several years later, he began to realize that he wasn't stupid. Within a year he was at the top of his class, and the hunger for knowledge had taken hold of him. It wasn't easy in the predominantly all-white school, though. After Ben received a certificate of achievement at the semester break, one of the school's teachers berated the white students for letting a black student get ahead of them academically.
Ben also had several teachers along the way who expressed a strong interest in his success. After he demonstrated his proficient knowledge of rocks in his 5th grade class, his teacher asked Ben to come by the school's lab after classes ended for the day. There Ben found squirrels to feed and a tarantula to observe. He discovered the wonders of using a microscope to study water specimens, and learned about paramecium and amoebas.
Later, at Southwestern High School in inner-city Detroit, his science teachers recognized his intellectual abilities and mentored him. Other teachers helped him to stay focused when outside influences pulled him off course.
After Ben graduated with honors from high school, he knew he wanted to pursue a medical career. But because his mother was not financially well off, Carson had to work through most of his time in college. The automobile industry was facing a downturn in Detroit during the 1970s, making it tough to get a summer job.
But Carson was determined to achieve his goals. He knocked on doors looking for summer work and usually, through persistence, was able to obtain one. From this work, and a scholarship, he attended Yale University and earned a B.A. degree in psychology.

MAPANGO YA AMBONI TANGA NA Hi5 MAKALA



Tanga ni mkoa mmoja wapo unaopatikana hapa Tanzania ukiwa katika pwani ya Afrika mashariki ya Bahari ya Hindi. Ni kilometa mia tatu Hamsini ukitokea (350 KM) Dar-es-salaam hadi Tanga. Mkoa huu kwakeli una mambo mengi yakihistoria kati ya mikoa maarufu sana enzi hizo Tanzania huwezi kuacha kuutaja mkoa wa Tanga. Team Hi5 Media ilifanikiwa kutembelea mkoa wa Tanga ambapo ilitembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria ikiwemo bandari kongwe ya Tanga, Mapango ya Amboni na kiwanda cha maziwa mpaka kule kwenye magofu ya kihistoria na katika kile kisiwa ambacho kinazama kinacho itwa Tongoni.


“YES GOOD BYE” ni maneno yaliyo tumiwa na bwana Osali Otango pindi alipokuwa akihudhuria mikutano ya wazungu pia alikazia kwa kusema “YOU WILL NEVER” pale wazungu wakikoloni walipo jadiliana jinsi ya kumkamata bwana huyu Osali Otango. Osali Otango alikuwa ni gwiji katika matumizi ya nguvu za giza mara zote alitafutwa na wakoloni wakizungu bila kupatikana. Osali Otango aliishi sehemu ya miujiza sehemu yakihistoria sehemu yenye mambo mengi ya kustaajabisha ambayo miaka milioni ishirini nyuma nazungumzia mapango ya amboni ama kwa jina la kisasa Amboni Caves. Mapango haya kwa sasa ni kivutio kikubwa cha utalii hapo mkoani Tanga. Katika mapango haya kuna mahali ambako watu walipatumia kuabudu na kufanya kafara wengi wao walikuwa ni makabila yanayo zunguka mapango haya yaani wazigua, wabondei pamoja na wadigo hapo zamani. Katika mapango haya kuna miamba inayo toka chini kwenda juu na inayotoka juu kuja chini kwa lugha ya kitaalamu wanajografia huita Slack tight na slug might pia kuna miamba inayo kutana na kutengeneza aina nyingine kabisa ambyo wanaiita Earth Pira.

Wanasema ukiyastaajabu ya musa utayaona ya firauni ndani ya mapango haya pana maumbo ya kijinsia, jinsia ya kike na jinsia ya kiume, pia kuna kiti cha asili kilicho chongwa na maji pamoja na kwato lakini pia ndani ya mapango haya kuna eneo ambalo dini ya kiislam na dini ya kikristo walikuwa wakipatumia kwa ajili ya kufanya ibada ama hakika mapango haya ni kivutio kikubwa sana.
Imeandikwa na Donald Mtani “The Super Voice” Hi5 Makala

MAVAZI YA MABINTI WA CHUO, NGONO INAHAMASISHWA



Serikali ikiwa inaendelea kupiga vita kuhusu mavazi katika jamii yetu tunayo ishi hususani katika swala la kutunza maadili na utamaduni wa kitanzania bado swala la mavazi yanayovaliwa na vijana wa kitanzania hayaridhishi. Mbali na sheria zilizo wekwa hivi karibuni ambazo zina ambatana na ukiukwaji wa mavazi yanayo valiwa pamoja na kuweka adhabu, faini au vyote lakini sheria hizi hazifanyi kazi. Wahenga wanasema mguu huvunjika ikiwa la mkuu halija sikilizwa sasa tujiulize hilo la mkuu ambalo halija sikilizwa wangapi guu zao zimekwisha vunjika.

Ukiachana na wakazi wa mtaani sheria hizi za mavazi zinakaziwa sana vyuoni maana ndiko tunategemea hawa wasomi baadae ndio watakao kuja kuwa viongozi wa baadae na wazazi pia, Je vipi swala la mavazi vyuoni lina fuatiliwa ipasavyo…? Wanachuo wengi mavazi yao hayaridhishi hasahasa kwa upande wa dada zatu maana ndio wengi wao wasema “tunaenda na fashion”. Fashion ambayo inawalizimu wavae nusu utupu au ni kisingizio, hapa tunakuja kugundua ni uhuru wanao upata maana wengi ni wakazi wa mikoani sasa wanapo fika ugenini kule wasiko julikana ndio chimbuko hili hukua na kuathiri na wengine.
Imekuwa kawaida ukipita mtaani kusikia “Aahh wasichana wa chuo ni Malaya” kwa kuwa mavazi wanayo vaa hayana tofauti na yale wanayovaa dada zetu wanao fanya biashara ya mwili ilo moja, Pili kwa wanaume ambao hupenda mabinti wa aina hiyo hujikuta wanavutiwa nao na hapa sasa mabint wa chuo wanafananishwa na ATM kwa maana kuwa ni sehemu ya  kutolewa pesa za muhusika kwa ajili ya matumizi yao tofauti. Unadhani kuhakikisha wana endelea kuvaa nguo za aina hizo ambazo ziko nje na bajeti za wazazi wao ama walezi zinatoka wapi, wanajikuta wanajirahisisha kwa wanaume ili tu waendelee kushindana kimavazi na wenzao wanapokutana chuoni.

Elimu inahitaji kuwa makini na kusoma pia kitabu hakihitaji mtu mwenye mambo mengi kwa maana ndio unatengeneza msingi wa maisha ya baadae, kwa mwenendo ambao dada zetu wanaendelea nao si rahisi mtu wa aina hiyo kuwa makini na masomo mwisho wazazi wanakuwa wamewekeza pesa zao kwenye kampuni hewa.