• This is Slide 1 Title

    This is slide 1 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 2 Title

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 3 Title

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Sunday, May 10, 2015

RAISI KIKWETE AWEKA SHADA LA MAUWA KABURI LA MASHUJAA ALGERIA







 R
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la mauwa kwenye kaburi la mashujaa Algeria Jumapili Mei 10, 2015

SHERIA YA MAKOSA YA JINAI YA MTANDAO YAANZA KUTUMIKA


POLISI HOI KWA KIPIGO, MBUNGE AKAMATWA

Loliondo. Polisi wawili, PC Isaack na PC Mabrouk wamejeruhiwa baada ya kupigwa na vijana wanaodaiwa kuwa ni Wamasai (morani) katika Kijiji cha Ololosokwani, Tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro.
Tukio hilo pia limesababisha watu 25 kutiwa nguvuni, akiwamo mbunge wa zamani wa Jimbo la Ngorongoro, Merthew ole Timan na madiwani wawili.
Inadaiwa tukio hilo limetokana na kuchochewa na uhasama kati ya wananchi na polisi kutokana na migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo, limesababisha PC Isaack kuvunjwa mkono na jana alihamishiwa Hospitali ya Seliani Arusha Medical Center kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kuwa mbaya.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Hashimu Mgandilwa alisema watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
“Ni kweli polisi wawili wamepigwa na jeshi liliendesha msako wa kuwatafuta watuhumiwa na kufanikiwa kuwakamata watu 25 kwa tuhuma za kushambulia polisi, uchochezi, kufanya mikusanyiko isiyo halali na kupanga mbinu za uhalifu,” alisema Mgandilwa.
Alisema chanzo cha kupigwa polisi ni operesheni ya kuchunguza wahamiaji haramu ambayo inapingwa na wananchi na viongozi wa eneo hilo.
Hata hivyo, viongozi waliokamatwa kuhusu tukio hilo, jana walipata dhamana.
Diwani wa Kata ya Ololosokwani, Iyanick Ndoinyo na Diwani wa Oldonyosambu Daniel Ngoitiko, walisema wanapinga tukio la kupigwa polisi hao, lakini chanzo ni polisi kukamata pikipiki za wananchi na kudai faini kubwa.
Iyanick alisema ingawa ni kweli kuna uhasama wa polisi na wananchi, lakini taarifa alizopata ni kwamba polisi wadai faini kubwa na kisha kumpiga kijana mmoja wa Kimasai.
“Sisi kama viongozi tunapinga kupigwa polisi, pia kukamatwa kwetu ni kudhalilishwa,” alisema.
Alisema, “Hatupingi hatua ya Serikali kuwaondoa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.”
Naye Ngoitiko alisema wao kama viongozi wanalaani tukio hilo na wanataka Serikali kufanya uchunguzi kujua chanzo badala ya kukamata watu bila kuwa na ushahidi.

Chanzo

Thursday, April 2, 2015

FRIDAY, PRINCE TOUZ KATIKA MAANDALIZI YA KICHUPA CHA MA LOVE DOVE

Wiki chache kupita baada ya moja ya muandishi wetu kutoka Hi5 Media huko Dodoma kufanikiwa kuwepo onset wakati Friday na Prince Touz wakiwa wanamulika kichupa cha Ma Love Dove alitujuza kuwa video hiyo itakuwa na ubora wa hali ya juu kulingana na maandalizi waliyoyafanya wasanii hao wawili.
Kushoto Friday kati Video Queen  Kulia Prince Touz               
Kwa mujibu wa muandishi wetu baada ya kufanya mahojiano na Prince Touz, "Kazi ni moja tu kuhakikisha mziki wetu unakwenda mbali zaidi na pia ni mda mrefu sana tulikuwa kimya sasa  ni Return of Friday na P Tanzania" alisema Prince Touz.
Prince Touz a.k.a Prince Tanzania akiwa kwa pouz
Friday moja kati ya Artist wanao fanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleiva sio tu DomTown even Tz mwenye radha ya pekee ila kwa mbali kama Bele flani ivi na ndie aliye pita zile radha flani za kuimba iv.....
Kulia Friday akiwa na moja kati ya wahusika katika Video
 Naam wadau wa muziki mkae tayari kupokea ujio mpya wa Friday na Prince Touz na huyu ndiye V.Q yaani Video Queen wa nyimbo ya Ma Love Dove
http://www.hulkshare.com/hi5music/friday-ft-prince-touz-ma-love-dove
Bofya hapa kusikiliza na kudownload nyimbo ya Ma Love Dove_Friday ft. Prince Touz

DIAMOND PLATNUMZ_NASEMA NAWE

https://www.youtube.com/watch?v=moE_dXt6-CQ
 Brand new mzigo toka kwa Diamond Platnumz inakwenda kwa jina la nasema nawe akiwa na nguli wa miondoko ya mirindimo ya pwani mwanamama bi Khadija Kopa ambapo mchupa umesimamiwa na mtu mzima Hanscana the Director him self Enjoy.

Thursday, March 26, 2015

WAGOMBEA WAAHIDI UCHAGUZI KUFANYIKA KWA AMANI NIGERIA



Wagombea wawili wa uchaguzi wa urais nchini Nigeria wameahidi kufanyika kwa uchaguzi wa amani,na kuongezea kuwa wataheshimu matokeo ya uchaguzi ulio huru na haki.
Rais Goodluck Jonathan pamoja na mpinzani wake wa karibu Muhammadu Buhari,pia wamewataka wafuasi wao kuiga mfano huo.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi baada ya kuahirishwa mwezi uliopita.
Mwandishi wa BBC amesema kuna wasiwasi kuhusu iwapo tume ya uchaguzi imejianda kusimamia uchaguzi huo na iwapo shughuli hiyo itaafikia matarajio ya wengi.

NDEGE ILIYO ANGUKA UFARANSA, ILIANGUSHWA MAKUSUDI



Rubani wa ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya jumanne alitaka kuiharibu ndege hiyo kulingana na maafisa wa Ufaransa.Kiongozi wa mashtaka katika mji wa Mersaille ,Brice Robin, akizungumza kulingana na habari aliyopata katika kijisanduku cha kunasa sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa ndani ya chumba cha kuendesha ndege pekee.


Rubani huyo kimakusudi aliishusha ndege hiyo kwa kasi huku rubani mwenza akiwa nje ya chumba hicho cha kuendesha ndege.
Bwana Robin amesema kuwa kulikuwa na kimya kikubwa ndani ya chumba hicho wakati rubani mwenza alipojaribu kuingia kwa nguvu.
Hatahivyo abiria walisikika wakipiga nduru kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo,aliongezea.
 
Rubani huyo kwa jina Andreas Lubtiz,mwenye umri wa miaka 28, alikuwa hai hadi wakati ndege hiyo ilipoanguka ,kiongozi wa mashtaka alisema.


Ndege hiyo aina ya Airbus 320 iliokuwa ikitoka Barcelona kuelekea Duesseldorf Ujerumani iligonga mlima na kuwauwa abiria wote 144 pamoja na wafanyikazi sita wa ndege baada ya kushuka kwa dakika nane.
"Tunasikia rubani akimuuliza rubani mwenza kuchukua udhibiti wa usukani wa ndege hiyo na vilevile tunasikia sauti ya kiti kikisonga nyuma na mlio wa mlango ukifungwa,bwana Robin aliwaeleza wanahabari.

UFISADI:KENYATTA AWASIMAMISHA 175



 Mawaziri 5, makatibu 6 wa kudumu na Magavana 10 wametajwa miongoni mwa maafisa 175 wa umma watakaolazimika kunga'atuka mamlakani katika siku 60 zijazo iliuchunguzi wa kina ufanyike kuhusu madai ya ufisadi dhidi yao. Hayo yalibainika katika ripoti iliyotolewa bungeni na rais Uhuru Kenyatta katika kikao maalum cha bunge la taifa kilichowajumuisha wabunge na maseneta.
Rais Kenyatta aliwataka maafisa wote wa umma waliotajwa katika ripoti hiyo waondoke ilituhuma zote dhidi yao zichunguzwe kwa kina na tume ya kupambana na ufisadi.
''Kwa hakika imewadia wakati ambapo serikali yangu haina budi ila kuchukua hatua mahsusi ambayo inalenga kukomesha hili zimwi la ufisadi mara moja''

UFISADI ''Ufisadi umevuka mipaka na lazima nasi tujifunge kibwebwe na kukabiliana nao''.
''Natarajia kuwa wale waliotajwa katika ripoti hii watanga'tuka mamlakani hadi pale uchunguzi utakapokamilishwa ndipo warejee afisini.'' alisema Kenyatta.
Kenyatta aliongezea kusema kuwa ''Ninamtaka kiongozi wa mashtaka ya umma kuanzisha uchunguzi mara moja kuhusiana visa vyote vilivyotajwa humu katika kipindi cha siku 60 zijazo''.


Ripoti hiyo iliyotayarishwa na tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya KACC inawadia wakati ambao kumekuwa na visa vingi vya ufisadi haswa katika serikali kuu na pia serikali za majimbo.
Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Kisa kilichozua mjadala ni kile cha 'Anglo Leasing'' ambayo ilijumuisha kandarasi za idara ya Uhamiaji idara ya upelelezi na Idara ya usalama wa taifa.
Mabilioni ya fedha yalilipwa kwa wanakandarasi waliotarajiwa kuwasilisha kazi ambazo hazikuwahi kufanyika hata wa leo.
Magavana 10 kati ya 47 wametajwa katika ripoti hiyo ambayo itatangwwa rasmi siku ya jumanne katika mabunge yote mawili.
Duru zinasema kuwa Kamati nzima ya bunge inayochunguza ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma imetajwa katika ripoti hiyo.
 MSAMAHA
Aidha Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Kenyatta alisema''ili wakenya waweze kusonga mbele na kusahau yaliyopita kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali zilizotangulia ni wajibu wangu
kuchukua fursa hii na kuwaomba msamaha wote waliodhulumiwa kwa njia moja au nyengine.
Zaidi ya Wakenya 650,000 walifukuzwa makwao kufuatia vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2008 na tume maalum ya haki ukweli na maridhiano TJRC
ilipendekeza kuwa sharti serikali iombe radhi kwani fedha haziwezi kufuta machungu ya mateso ambayo wakenya wamepitia''
''Hata hivyo licha ya mapendekezo ya tume hiyo ya maridhiano,nimeagiza wizara ya fedha itenge shilingi bilioni 10 dola milioni 110, katika kipindi cha miaka
mitatu ijayo kwa ajili ya kuwafidia wale wote walioathirika''

TAMASHA LA MUZIKI KENYA



Nchini Kenya, ni wakati wa tamasha la sanaa ambapo shule na vyuo vinashindana.
Maelfu ya wanafunzi hukusanyika kuonesha vipaji vyao katika sanaa za utamaduni.
Muhimu tu washinde tuzo. Na si rahisi kwani wavulana ni wasichana na wasichana ni wavulana.