• This is Slide 1 Title

    This is slide 1 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 2 Title

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 3 Title

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Thursday, November 13, 2014

Blog Hi5: JXJ AKIFANYA YAKE KATIKA JUKWAA LA KONGWA AFRIKA P...

Blog Hi5: JXJ AKIFANYA YAKE KATIKA JUKWAA LA KONGWA AFRIKA P...: Moja kati masaani wa Muziki wa Kizazi kipya anayefanya vizuri katika kazi zake ambaye yuko chini ya lebo ya DomTown Records JX, hapo akiwa...

JXJ AKIFANYA YAKE KATIKA JUKWAA LA KONGWA AFRIKA PAMOJA PROJECT

Moja kati masaani wa Muziki wa Kizazi kipya anayefanya vizuri katika kazi zake ambaye yuko chini ya lebo ya DomTown Records JX, hapo akiwa anafanya yake katika show iliyo andaliwa na kampuni ya Akonshaz Music ndani ya kitengo cha Muziki chini ya project ya Afrka Pamoja

DENI LA BILIONI 102 MSD: SERIKALI YAWEKWA KITIMOTO BUNGENI

MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, mkoani Rukwa, Bw. Ally Mohamed Kessy (CCM), ameitaka Serikali itoe tamko la haraka kuhusu hali ya upatikanaji huduma za afya katika hospitali za umma.
Alisema hivi sasa maafa yanayowapata Watanzania kutokana na uhaba wa dawa katika hospitali na vituo vya afya vilivyopo chini ya Serikali ni zaidi ya vifo vilivyotokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea nchini Rwanda na Burundi.
Bw. Kessy aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana baadaya kuomba mwongozo na kusisitiza kuwa, hali ya upatikanaji dawa katika hospitali na vituo vya afya ni mbaya.
“Madhara yanayotokana na ukosefu wa dawa ni zaidi ya vita vilivyotokea Rwanda na Burundi... naiomba Serikali iache mzaha na suala hili, itoe tamko haraka ili Watanzania wajue la kufanya,” alisema Bw. Kessy.
Siku chache zilizopita, Mbunge wa Kisesa, mkoani Simiyu, Bw. Luhaga Mpina, alilitaka Bunge kusitisha vikao vyake ili fedha zinazotumika kuwalipa posho, zitumike kulipa deni ambalo Serikali inadaiwa na Bohari ya Dawa (MSD).
Deni hilo ni sh. bilioni 102 hali inayosababisha MSD ishindwe kumudu gharama za kuagiza dawa nje ya nchi.
Akisisitiza msingi wa hoja yake, Bw. Kessy alisema kutokana na tatizo hilo, Watanzania wengi wanapoteza maisha hasa watoto na wajawazito; hivyo ni vyema Serikali ikatoa tamko la kupatikana ufumbuzi wa tatizo hilo haraka iwezekanavyo.
Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya, alisema mashine ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi katika Hospitali ya Ocean Road, ni mbovu isipokuwa moja ambayo nayo inafanya kazi kwa kusuasua hali ambayo inasababisha mateso makubwa kwa wagonjwa wanawake.
“Hadi sasa, hali ya huduma za afya pale Ocean Road ni tete, mashine ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi imekufa, inayofanya kazi ni moja tena kwa kusuasua...Serikali itoe tamko ili kunusuru maisha ya wanawake, hali ni mbaya,” alisema.
Akitoa ufafanuzi wa suala hilo kwa niaba ya Serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandyosa, alisema suala la tiba ni muhimu kwa uhai wa binadamu ambapo Serikali inatambua tatizo lililopo.
Alisema Serikali itatoa tamko rasmi bungeni hivyo aliwaomba wabunge kuwa na subira ambapo Prof. Mwandosya, pia alitolea ufafanuzi kuhusu mwongozi ulioombwa na Mbunge wa Mbozi Magharibi, mkoani Mbeya, Bw. David Silinde (CHADEMA).
Katika mwongozo huo, Bw. Silinde alitaka Serikali itoe tamko kuhusu madeni ya wakulima wa mahindi waliyouza kwa Wakala wa Hifadhi ya Taifa (NFRA), yaliyodumu kwa miezi mitatu lakini Serikali imekaa kimya bila kutoa kauli yoyote.
Bw. Silinde alisema wakulima hao wamelima mahindi na sasa hawanufaiki nayo kwani mbali na kuendelea kuidai Serikali, mengine yanaoza kwa kukosa soko na kuwasasabishia umaskini.
Akijibu hoja hiyo, Prof. Mwandosya alisema ni kweli suala la wakulima wa mahindi limezungumza sana ambapo Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, itatoa tamko la Serikali wiki hii.

Bunge hilo liliendelea kujadili mpango wa maendeleo ambapo Mbunge wa Mbeya Mjini, Bw. Joseph Mbilinyi (CHADEMA), alidai kusikitishwa na kauli aliyoiita nyepesi.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe kuhusu kuenea kwa habari za Rais wa China kuondoka na meno ya tembo alipokuja nchini.
Alisema Bw. Membe alitoa kauli nyepesi ambayo kila akiitafakari anashindwa kuelewa hasa ukizingatia suala hilo ni nyeti na linagusa masilahi ya Taifa; hivyo alistahili kulieza Bunge kwa umakini si kama alivyofanya.
“Nimesikitishwa na kauli ya Waziri Membe, nilitegemea kuona akiliambia Bunge hatua zilizochukuliwa na Serikali au kuunda tume ili iweze kubaini ukweli wa jambo hilo badala ya kutoa taarifa za kukanusha bungeni.
“Mbali ya Rais wa China kuchafuliwa, Taifa letu pia limechafuka kwa sababu suala hili limezungumzwa katika vyombo vya habari ambavyo vingi ni vya kimataifa,” alisema.