• This is Slide 1 Title

    This is slide 1 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 2 Title

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 3 Title

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Wednesday, October 22, 2014

TAFAKARI

Tafakari...!

TANZANIA KUPATA NEMBO YAKE YA BIASHARA



MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tan Trade), ipo katika mchakato wa kuandaa nembo ya kibiashara itakayoitambulisha na kuitangaza Tanzania katika suala zima la uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika mkutano wa mchakato wa kupata usajili wa kuwa na nembo mpya ya Taifa, Mkurugenzi wa Tan Trade, Jacqueline Maleko, alisema kuwa ni vema ifikapo mwakani wakapata usajili  utakaosaidia taifa kuwa na nembo  yake.
Alisema endapo watafanikiwa kupata usajili Tanzania itatangazika katika uwekezaji na kwamba hakuna nchi itakayoweza kujitambulisha kibiashara kwa kutumia rasilimali za taifa.
Maleko aliongeza kuwa  Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo pia ni adimu kupatikana katika nchi  nyingine yeyote duniani na kwamba baadhi ya nchi zikifanya upotoshaji wa makusudi na  kujitangaza kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini.
Aliongeza kuwa  licha ya  mchakato kuwa na changamoto zake kwa kuhitaji  fedha nyingi mamlaka yake itahakikisha  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanafanikisha suala hilo alilolitaja kuwa ni  kilio chao cha muda mrefu.
Maleko alisema katika kuhakikisha wanafanikiwa katika azma hiyo ya kupata nembo ya Taifa ya kibiashara mamlaka yake itashirikiana na  kampuni ya Squire Patton Boggs kutoka nchini Marekani.
Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama   wa Tanzania  (TPSF),  Geofrey Simbeye alisema nchi imechelewa  kupata nembo ya  taifa na kwamba suala hilo lilipaswa kufanywa miaka 10 iliyopita na kuwataka wadau kuhakikisha suala hilo

MADEREVA, MAKONDAKTA UDA KUKIONA



ABIRIA wa mabasi jijini Dar es Salaam, wameshauriwa kusaidia kudhibiti uendeshaji holela na tabia zisizokubalika zinazofanywa na baadhi ya madereva na makondakta kwa kupiga simu zilizochapishwa katika mabasi yote ya Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA).
Taarifa ya UDA iliyotolewa jijini Da es Salaam jana na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, George Maziku, ilieleza kuwa utumiaji wa namba hizo utaisaidia pia kampuni kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja wake.
“Tunawakumbusha wateja wetu pamoja na watumiaji wengine wa barabara kuripoti uzembe wowote au utovu wa nidhamu utakaofanywa na madereva na makondakta wa UDA, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
“Mbali na kuboresha utoaji wa huduma zetu, UDA inalenga kuwa mfano wa kuigwa kwa mabasi mengine ya abiria nchini katika uzingatiaji wa sheria, utoaji wa huduma nzuri kwa wateja na kuwa kichocheo cha kupunguza foleni katikati ya jiji la Dar es Salaam,” alisema.
Maziku alisema uongozi wa UDA utachukulia kwa uzito mkubwa na kuyafanyia kazi maoni yote yakayokuwa yakitolewa kupitia namba hizo, ili kuondokana na dhana potofu kwamba wamiliki na waendeshaji wa kampuni za magari ya abiria ni watu ambao hawajaelimika.
Alisema  mbali na uwepo wa namba hizo za simu, UDA itaendelea na utekelezaji wa utaratibu wake wa kutuma waratibu kupanda mabasi ya kampuni hiyo na kuripoti juu ya utendaji kazi wa madereva na makondakta wa mabasi hayo.