• This is Slide 1 Title

    This is slide 1 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 2 Title

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 3 Title

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Sunday, April 24, 2016

TAKUKURU Kuchunguza Mabilioni ya Kikwete


ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza kuchunguza fedha za uwezeshaji maarufu kama ‘Mabilioni ya JK’ ambazo hazikurejeshwa na wakopaji nchi nzima. 

Msemaji wa Takukuru, Tunu Mleli alisema jana kuwa taasisi hiyo imechukua jukumu hilo kwa sababu moja ya majukumu yake ni kuchunguza masuala ya rushwa na kutoa rai kwa mtu mwenye ushahidi au taarifa kuhusu suala hilo kuzitoa kwa taasisi hiyo.

“Takukuru ipo wazi kuzipokea taarifa hizo ili zitusaidie kwenye uchunguzi,” alisema Tunu.

Kati ya Sh50 bilioni zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, ni Sh43 bilioni tu zilizorejeshwa, huku Sh7 bilioni zikidaiwa kutafunwa. 

Fedha hizo zilitolewa na Kikwete kwa ajili ya kuwawezesha kimitaji, wajasiriamali nchi nzima, mikopo ambayo ilipitia benki za CRDB, NMB, Community Bank na Benki ya Posta Tanzania. 

Fedha hizo kutoka Mfuko wa Rais, zilikuwa zikikopeshwa kwa riba ya asilimia 10, ambapo asilimia mbili ilikuwa inaingia serikalini na nane ilikuwa inabaki kwenye benki hizo. 

Hata hivyo, baadhi ya vyama vya Akiba vya Kuweka na Kukopa (Saccos), vilivyopewa fedha hizo, vilitoa mikopo hiyo kiholela, huku baadhi ya viongozi wakidaiwa kutengeneza majina feki na kukopeshana fedha hizo. 

Imedaiwa kuwa Saccos nyingi ambazo zilifuja fedha hizo katika mikoa mbalimbali, viongozi wake wengi walikuwa pia ni viongozi wa kisiasa na wengine wakiwa na nyadhifa serikalini. 

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, baadhi ya waliokopeshwa fedha hizo na Saccos mbalimbali, hawakuwa wanachama, bali walichomekwa baada ya kuonekana kuna fursa ya ‘kupiga dili’.

Chanzo kutoka Takukuru, kimedokeza  kuwa makamanda wa taasisi hiyo katika mikoa mbalimbali, wamepewa maelekezo ya kuchunguza mahali yalipo mabilioni hayo na nani waliyafuja.

 “Ni kweli tumepewa maelekezo ya kuchunguza fedha hizo. Unajua hizi ni fedha za umma haziwezi kutafunwa tu hivihivi na Serikali ikakaa kimya,” alidokeza mmoja wa maofisa wa Takukuru. 

Machi mwaka jana, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Christopher Chiza aliagiza kufanyika kwa ukaguzi wa kina wa fedha hizo.

Alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (Neec), ambako aliagiza watakaobanika kuhusika na ubadhirifu wa fedha hizo wachukuliwe hatua za kisheria.

“Lazima tuangalie mabilioni ya JK yalipotelea wapi, yalivyofujwa na wahusika wapo wapi ili sheria ichukue mkondo wake. Nimeambiwa kuna zilizobaki tujue ziko wapi,”alikaririwa Chiza akisema. 

Lakini Desemba 24, 2013, mtangulizi wa Chiza, Mary Nagu alikaririwa akisema Sh43 bilioni kati ya Sh50 bilioni za mabilioni ya JK zilizokopeshwa kwa wajasiriamali 74,701 zilikuwa zimerejeshwa. 

Nagu alitoa takwimu hizo alipokuwa akizungumzia mafanikio ya Serikali ya Rais Kikwete katika, utaratibu uliofanywa pia na wizara nyingine. 

Suala la mabilioni hayo ya JK limekuwa likiibuka mara kwa mara bungeni na katika mitandao mbalimbali ya kijamii huku wananchi wakitaka zirejeshwe.

Mkataba wa Lugumi

Hii hapa ni taarifa ya Utekelezaji Ya Kamati Ndogo ya PAC Kuhusu Mkataba wa Lugumi


NAPE KUDILI NA MAJIPU KWENYE SANAA


Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na michezo nchini,Nape Nnauye ametaja mambo manne ambayo ni vikwazo ndani ya sekta ya sanaa ya filamu nchini na kuyaita kwamba ni majipu huku akisisistiza kwamba serikali itakwenda kutunga sera ya sekta hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17.

Nape,aliyataja mambo hayo na kuyafananisha na majipu kuwa ni uporaji wa kazi za wasanii nchini,ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii nchini,usimamizi mbovu wa bodi ya filamu nchini sanjari na tatizo la mfumo mbovu wa usambazaji wa kazi za wasanii nchini.

Akizindua tamasha la filamu la Tanzanite International Film

Festival(TIFF) jijini Arusha juzi ambao ulihudhuriwa na wasanii maarufu wa filamu nchini waziri huyo alisema kwamba jipu la kwanza ambalo atakwenda kulitumbua ni uporaji wa kazi za wasanii nchini.

 

“Jipu la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka 2016/17 ni uporaji wa kazi za wasanii nchini wengi wananyonywa jasho lao”alisema

Nape

Hatahivyo,alisema kwamba jipu la pili ni ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii za filamu nchini na kudai kwamba chini ya uongozi wake atahakikisha anaimarisha miundombinu bora kwa lengo la kuwasaidia wasanii hao pamoja na kulinda haki zao.

Alisema ya kwamba mfumo wa kazi za usambazaji wa kazi za wasanii nchini pamoja na hakimiliki ni wa kinyonyaji huku akitolea mfano wa kazi za msanii maarufu wa sanaa hiyo nchini marehemu Stephen Kanumba na kusema kwamba familia yake hainufaiki na matunda ya kazi zake hadi sasa kutokana na mfumo mbovu wa usimamizi wa kazi za wasanii nchini.

Alitaja takwimu kwamba mwaka 2011/12 jumla ya filamu 218

zilitengenezwa nchini na mwaka 2014/15 kazi hizo ziliongezeka hadi kufikia 14,00 huku akidai hilo linadhihirisha kwamba sekta hiyo inakua kwa kasi nchini na kuongeza ajira 
 

Hatahivyo,Rais wa shirikisho la wasanii wa filamu nchini(TAFF),Simon Mwakifamba aliwataka wasanii wa filamu nchini kujiandaa kisaikolojia kukabiliana na soko la ushindani wa filamu duniani kwa kuwa wabunifu.

“Serikali tunaiomba iandae sera itakayoandaa mazingira mazuri kwa wasanii nchini kuhusu usalama wa kazi zao”alisema Mwakifamba

Naye, muaandaji wa tamasha hilo,Said Sassi alisema kwamba tatizo la uharamia wa kazi za wasanii nchini limetanda na kuwaomba wafanyabiashara na makampuni kujitokeza kudhamini vipindi mbalimbali vya luninga kwa lengo la kuinua sekta hiyo.

Mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya vito ya Tanzanite One Mining Ltd ambao ni miongoni mwa wafadhili wa tamasha hilo,Feisal Shabhai alisema lengo la kampuni yao kujitosa kufadhili tamasha hilo ni kutoa mchango wao katika kusaidia jamii kupitia faida wanayoipata ili kuinua sekta ya ajira nchini.

KIZIMBANI KWA KUHIFADHI WAHAMIAJI HARAMU


Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Simon Kagoli amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuhifadhi wahamiaji haramu nyumbani kwake na kuwatumikisha mashambani.

Kagoli ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kageji, anakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kuishi na watu ambao sio raia, kuwasaidia raia wa kigeni kutenda kosa na kuajiri na kuwatumikisha wageni shambani mwake. Kesi hiyo namba 114/2016 iko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Kibondo, Robert Male.

Mwendesha Mashitaka wa Uhamiaji, Richard Mwangole alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa makusudi huku akijua kuwa kuhifadhi wahamiaji haramu ni kosa kubwa. Anatuhumiwa kuwafanyisha kazi wahamiaji hao na kuwalipa ujira wa Sh 110,000 kila mmoja. Male alikana makosa na yuko nje kwa dhamana.

Alidhaminiwa na wadhamini wawili, kila mtu kwa dhamana ya Sh milioni moja.

Serikali ya China kudhibiti dini

Chama cha kikoministi cha China kimepewa mamlaka ya kudhibiti dini nchini humo.

Kiongozi wa Uchina, Xi Jinping, amesema makundi ya kidini lazima yakubali kudhibitiwa na chama cha kikoministi.

Akizungumza katika mkutano wa siku mbili mjini Beijing,rais Xi alisema itikadi za dini lazima zifuate sheria na utamaduni wa Uchina.

Alisema dini haina mchango katika siasa za nchi.

Rais Xi piya alionya watu wa nje wanaingilia kati ya mambo ya taifa kwa kupitia njia za kidini.

Watu wa Uchina wanahimizwa kuhudhuria maeneo ya ibada yaliyokubaliwa na taifa na wanaweza kutiwa adabu kali wakifanya ibada kinyume cha sheria.

Serikali ya China kudhibiti dini

Chama cha kikoministi cha China kimepewa mamlaka ya kudhibiti dini nchini humo.

Kiongozi wa Uchina, Xi Jinping, amesema makundi ya kidini lazima yakubali kudhibitiwa na chama cha kikoministi.

Akizungumza katika mkutano wa siku mbili mjini Beijing,rais Xi alisema itikadi za dini lazima zifuate sheria na utamaduni wa Uchina.

Alisema dini haina mchango katika siasa za nchi.

Rais Xi piya alionya watu wa nje wanaingilia kati ya mambo ya taifa kwa kupitia njia za kidini.

Watu wa Uchina wanahimizwa kuhudhuria maeneo ya ibada yaliyokubaliwa na taifa na wanaweza kutiwa adabu kali wakifanya ibada kinyume cha sheria.

Wakenya kinara katika London Marathon

Mwanariadha mkenya Eliud Kipchoge nusura avunje rekodi ya duniaya mbio za Marathon alipoandikisha muda wa kasi zaidi katika mbio za London Marathon.

Kipchoge wa Kenya,alihifadhi taji aliloshindwa mwaka uliopita alipoandikisha muda wa kasi zaidi wa saa mbili dakika tatu na sekunde 5 sekunde 8 tu nje ya rekodi ya dunia ya mbio hizo.

Rekodi hiyo ya dunia iliwekwa na mkenya mwenza Dennis Kimetto katika mashindano ya Berlin Marathon mwezi Septemba mwaka wa 2014.

Kipchoge ambaye alikuwa ameandamana na mkenya mwenza Stanley Biwott hadi iliposalia takriban kilomita tatu kufikia kwenye utepe , alipotifua kivumbi na kubaini udedea wake katika mbio hizo za masafa marefu.

Biwott alijifurukuta na kumaliza katika nafasi ya pili huku mpinzani wake katika mbio za mita 5000 Kenenisa Bekele kutoka Ethiopia akifunga orodha ya tatu bora.

Kufuatia ushindi huo Kipchoge ndiye mwanariadha wa kwanza tangu Martin Lel vilevile wa Kenya aliposhinda taji lake la pili mwaka wa 2008.

Katika kitengo cha wanawake cha mbio hizo ,Mkenya mwengine, Jemima Sumgong, aliyeanguka katika sehemu ya mwanzo mwanzo wa mashindano ya leo alijitahidi na kuibuka mshindi wa mbio za wanawake.

Sumgong, 31, aligonga kichwa chake chini baada ya kutegwa na mwanariadha mpinzani kutoka Ethiopia Aselefech Mergia.

Hata hivyo alijifurukuta kutoika nyuma na kuandikisha muda wa saa mbili dakika 22 na sekunde 58 alipokata utepe na kutawazwa bingwa mwaka huu wa mbio za London Marathon.

Tigist Tufa wa Ethiopia, aliyeshinda mwaka jana, safari hii amekuwa wa pili.

Mkenya mwengine Florence Kiplagat alimaliza katika nafasi ya tatu akitumia muda wa saa mbili dakika 23 na sekunde 39

NAPE AZINDUA TAMASHA LA KIMATAIFA LA FILAMU MJINI ARUSHA

 Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani Arusha .

 Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha hilo kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwenye historia ya filamu nchini na kuahidi Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha haki za wasanii hazipotei wala haziliwi na wajanja.

 

 Mkurugenzi wa Tanzanite One ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha, Ndugu Faisal Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mjini Arusha kwenye hotel ya Mt. Meru

  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifunua pazia kuashiria uzinduzi wa Tamasha la kimataifa la filamu la Tanzanite mjini Arusha.

  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Ntibenda  kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wadhamini kwenye uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite.

 Viongozi wa Arusha wakiwa

 Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite.

Yvonne Cherry 'Monalisa' pamoja na mama yake, Suzan Lewis 'Natasha' (katikati) wakifuatilia sherehe uzinduzi wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite kwenye hotel ya Mt. 

UKIMYA WA UPINZANI BUNGENI MASHAKA KWA WASOMI



UAMUZI wa Kambi ya Upinzani bungeni kuingia katika vikao vya Bunge na kugeuka bubu wakati wa mjadala wa Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, umechukuliwa kwa hadhari kuwa unaweza kusababisha kambi hiyo ionekane inalinda posho bungeni.

Hadhari hiyo imetolewa na wasomi na viongozi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili jana, walipokuwa wakitoa maoni kuhusu uamuzi wa kambi hiyo kususa hotuba hiyo.

Dk Bana

Mhadhiri wa fani ya siasa na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, ndiye aliyesema kuwa kama uamuzi huo wa kuwa bubu bungeni hautabadilishwa, kambi hiyo itaonekana inalinda posho na kwamba haipo kwa ajili ya kutetea wananchi.

“Kazi yao ni kuwakilisha wananchi na makundi yote bungeni, sasa kitendo cha kuota ububu na kushindwa kueleza kero za wananchi, ni kutotendea haki wananchi maana ni vema wakae bungeni na kutoa hoja zao la sivyo, itafika wakati watatuomba radhi wananchi,” alisisitiza.

Akizungumzia hoja ya kwanza ya Mwenyekiti wa kambi hiyo, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), kulalamikia muundo wa Serikali kutowekwa gazetini, Dk Bana alihoji kama Mbowe hajui kuwa muundo wa Serikali hautolewi kwa kila mtu.

Kuhusu suala la fedha zilizokatwa katika Mfuko wa Bunge na kuelekezwa katika utengenezaji wa madawati, Dk Bana aliwashangaa wawakilishi hao wa wananchi wanaopingana na uamuzi wa kumuinua mwananchi wa kawaida.

Alisema wananchi wote walipendezwa na hatua hiyo ya Serikali ya kuchukua fedha zilizotoka bungeni baada ya kubana matumizi na kupeleka katika kununua madawati.

“Hatua hii ni kielelezo kuwa Bunge lilikuwa likipangiwa fedha nyingi kuliko matumizi yake hivyo kusababisha kuwepo matumizi ya hovyo, sasa viongozi wa Bunge kuliona hilo na kurejeshwa kwenye jamii ni jambo jema,” alisema.

Alionya kuwa mikakati ya kambi ya upinzani, ni kutetea wananchi lakini kwenye hilo wananchi wenyewe kila kona wanawashangaa kwani inaonesha kutetea maslahi ya wabunge.

Bashiru Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally alisema wananchi wanaangalia vitendo vya wabunge wao ndani ya Bunge na watawahukumu kwani michango yao ndani ya Bunge ni muhimu na njia ya kutatua tatizo si kususa, bali kufuata taratibu za kisheria.

Alisema uamuzi wa kutozungumza, unaondoa maana ya vyama vya upinzani ndani ya Bunge kwa kuwa watashindwa kujadili masuala yenye manufaa ya wananchi, kwani mawazo ya kiongozi wa upinzani bungeni ni muhimu na yanawekwa kwenye kumbukumbu.

“Kuwekwa kwenye kumbukumbu mawazo hayo ni kwa ajili ya vizazi vijavyo, sasa kitendo cha Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kutumia vibaya nafasi anayopewa, ni udhaifu wa kimkakati,” alisisitiza Bashiru.

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alisema wanavyofanya wapinzani ni jambo lisilopendeza katika kuleta umoja wa kitaifa, kwani wao ni wawakilishi wa wananchi ndani ya Bunge na kususa siyo jambo la kiungwana.

TWITTER YAMTIA NDANI MWANDISHI


Polisi nchini Uturuki wamekamata mwandishi wa habari aliyemkosoa rais wa nchi hiyo kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.

Ebru Umar raia wa Uholanzi alikamatwa na polisi baada ya kumkosoa rais Recep Tayyip Erdogan alikamatwa katika mji wa wa magharibi wa Kusadasi jumamosi usiku.

Wizara ya maswala ya nje ya Uholanzi imethibitisha kuwa Bi Umar alichapisha ripoti iliyomkosoa Sera za rais Erdogan ya kuwataka watu wote wenye asili ya Uturuki kuripoti wakati wowote mtu anapomtusi au kumkosoa nchini Uholanzi.

Hapo jana rais wa baraza kuu la muungano wa ulaya Donald Tusk, aliitaka serikali iruhusu uhuru wa kujieleza kama inavyotakikana kikatiba itakelezwe.

Tusk ambaye alikuwa ameandamana na waziri mkuu Ahmet Davutoğlu alionya kuwa uhuru wa wanahabari unatishiwa na maamuzi ya wanasiasa wachache serikalini.

Bw Davutoğlu kwa upande wake ameamua kutetea rekodi ya Uturuki, kuhusiana na uhuru wa vyombo vya habari, katika kikao na waandishi habari kilichohudhuriwa na Bi Merkel na maafisa wakuu wa jumuia ya muungano wa bara Ulaya.

Rais wa baraza kuu la muungano wa jumuia ya EU Donald Tusk, alidokeza kuwa, wanasiasa wanafaa kuamua kuhusiana na swala la ukosoaji na uharibifu wa hadhi ya mtu, hasa kuhusiana na ukiukaji wa haki ya uhuru wa kujieleza kwa vyombo vya habari.

Baadhi ya wanahabari wa Uturuki wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kutoa siri za serikali.

Mwezi uliopita, gazeti kuu linaloandika maswala ya upinzani - Zaman, lilishuhudia wanachama wa halmashauri kuu ya usimamizi, wakifutwa kazi na mahala pao kujazwa na waandishi, wanaounga mkono serikali.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan pia, amekuwa akitathmini kuwasilisha mashtaka dhidi ya muigizaji wa kuchekesha, raia wa Ujerumani, ambaye alitoa matamshi ya kumkejeli.

BURIANI PAPA WEMBA

Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- Papa Wemba amefariki dunia

Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.

Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.

Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous,

Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani.

Msanii huyo nguli mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni anasemekana alianza kutetemeka, kisha akaanguka na kuzirai, alipokuwa akitumbuiza jukwaani Abidjan.

Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake, alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.

Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele, Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na " Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) , "Zania" (Mavuela Somo.

UGANDA: BOMBA LA MAFUTA KUPITIA TANZANIA


Uganda imeamua kujenga bomba la mafuta yake kupitia Tanzania na wala sio Kenya.

Awali taifa hilo la Afrika mashariki ambayo haijapakana na bahari ilikuwa imezungumzia nia ya kujenga bomba la mafuta yake kupitia Kenya lakini baada ya mkutano na rais wa Tanzania Joseph Pombe Magufuli, rais wa Uganda Yoweri Museveni wameibwaga Kenya.

Kenya ambayo imegundua mafuta Kaskazini mwa taifa hilo sasa haina budi kujiunga na uganda kupitishia mafuta yake Tanzania au ijenge bomba lake kupitia bandari ya Lamu.

Uganda imeelezea wasiwasi wa mabomba ya mafuta kushambuliwa na wanamgambo wa Alshabab kwani bomba hilo la kupitia Kenya linatazamiwa kutumia bandari ya Lamu.

Uganda ilitangaza uamuzi wake katika kongamano la viongozi wa muungano wa Afrika Mashariki uliokuwa mji mkuu wa Kampala.

Muungano huo unajumuisha Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini.

Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga.

Mradi huo utagharimu takriban dola bilioni $4 za Marekani.

Aidha ujenzi huo unatarajiwa kutoa nafasi za kazi 15,000 kwa vijana ambao wanatatizika sana na uhaba wa ajira.

Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga.

Uganda inakisiwa kuwa na mapipa bilioni 6.5 bn ya mafuta yanayotarajiwa kuanza kuchimbwa mwaka wa 2018.

Kampuni ya mfuta ya Ufaransa Total, ile ya China CNOOC na ile ya Uingereza Tullow ndizo zinazomiliki leseni ya kuchimba na kusafisha mafuta nchini Uganda.

Kenya sasa imeamua kujenga bomba lake kufuatia uamuzi huo wa Uganda.