Wednesday, July 9, 2014

PICHA ZA UTUPU MTANDAONI NA MABINTI WAKITANZANIA


Hivi ndivyo jamii ya kitanzania inavyo jilea maika ya sasa huku shutuma nyingi zikielekezwa katika matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii pasi na kuchunguza nini chanzo ama sababu kubwa inayo pelekea jamii yetu yakitanzania kusahau maadili yetu. Tuanze na kujiuliza hivi ni kwanini maadili yana momonyoka kila leo, zamani enzi za mababu zetu si kwamba hakukuwa na maadili mabovu lakini kulingana na kwamba utandawazi umeifanya dunia kuwa kijiji mengi yanayofanyika kwa siri sasa hayana sehemu yakufichwa. Moja kati ya jinsia inayo jaliwa sana karibu kwa kila sekta ni jinsia ya kike na si kwa Tanzania tu hii ni sera ya dunia nzima lakini dada zetu ama mabinti wa kiafrika hususani wakitanzania wamekuwa wakijishusha hadhi na heshiama wanazopewa katika jamii kwa mambo wanayo fanya sasa, kabla hatuja anza kugusia yanayo endelea kwenye mitandao sasa mpendwa msomaji wangu nikujuze jambo moja kwanza, kabla ya hata mabinti hawa wachache kuanza kutupia ndani zao nje walianza na mavazi yasiyo stahili ambayo yanaweka karibu robo tatu ya mwili nje sasa kila jambo huanza likiwa dogo tukaanza kuona post mbalimbali za picha zao za wilu (utupu) zikiwa hadharini eti zimeliki wengine wapenzi wao wamezitoa kisa wameachana mpaka sasa wana amua wenyewe kujipiga na kuziweka kwenye mtandao.


Ona jinsi mzunguko ulivyo unamiliki simu yenye uwezo mzuri wa kupiga picha kisha simu hiyo ina apps tofauti za kimtandao zinazo ruhusu kufanya system data uploading  hapa namaanisha Instagram, whattsapp, facebook ambapo baada yakujipiga picha ukiwa ndani kwako then mtu huyo anapost picha hizo kwa mtandao alafu baadae tuseme zimeliki au mmoja amezivujisha. Muda mwingine bishara nayo huitaji matanazo ili iweze kutoka sasa tuangali je ni kosa la mtandao au watumiaji wenyewe maana mtandao huohuo unamfanya mtumiaji kufaulu huko mavyuoni kwa kusafu material mbalimbali na ndio mtandao huohuo unaofanya mtumiaji kupost picha zake za utupu. Pengine ni uhuru binafsi wa matumizi haya ya mtandao au ni kuto kuwepo na mfumo  wauzuizi wa vitu vya kuonekana kwenye mtandao, pia hili halifatiliwi sana kwa maana wako wakubwa ama wanene wanopenda kuona vitu hivyo ili wajue wapi pa kuchepukia. Amini kitu kimoja katika namba ikipungua au kuongezeka moja basi mahesabu hayawi sahihi sasa hata haya tunayo yaona au kuonekana kwenye mtandao ya athiri sana jamii yetu na kuipeleka kusiko sahihi.

0 comments:

Post a Comment