Wednesday, July 9, 2014

STORI YA SNURA WA MAJANGA


Snura Mushi ni binti mwenye vipaji vingi ndani ya tasnia ya bongo movies. Pamoja na kuwa mwigizaji aliyekuja kwa kasi sana pia Snura ni mwanamuziki wa bongo fleva anayefanya vizuri sana sokoni kwa nyimbo zake mbalimbali zenye mahadhi ya pwani mithili ya mduara. Pamoja na kuwa na umbo na sura nzuri ya kuvutia snura pia amekuwa akitawala sana vichwa vingi vya habari,magazeti na redio kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukata kiuno kwenye nyimbo zake.
Snura Mushi (Jina lake halisi) alizaliwa tarehe kumi na mbili (12) mwezi wa kwanza (1) mwaka 1984 Jijini Dar es salaam ambako aliweza kukua na kupata elimu yake hapo hapo Dar es salaam.


Tofauti na watu wengi wanavyofahamu,kipaji cha mwanadada Snura  kilianzia kwenye muziki kabla ya kuigiza na alikuwa na mwimbaji wa taarabu na kundi la “new best star” mwaka 2004. Baada ya hapo alianzisha kundi lake la muziki aliloliita “chanya na hasi” pamoja na vijana wawili mmojawapo akiwa marehemu sharo Milionea kabla hajajiunga rasmi na sanaa ya maigizo. Kipaji cha mwanadada Snura Kiligunduliwa na mtu aliyefahamika kwa jina la Siasa. Ambaye ndiye aliyemfuata na kumshauri kuigiza baada ya kuvutiwa na uzuri na umbo lake ambalo kwa mujibu wa mtu huyo alikuwa na “star look” na angeweza kufanya vizuri kama angejiingiza katika sanaa. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2006. Na mwaka huo alipata nafasi ya kuigiza kwenye Filamu ya Mfalme Seuta iliyodirectiwa na Gumbo Kihorota. Baadaye aliweza kucheza movie za Zinduna na Hitimisho.

Snura alianza kujipatia umaarufu sana kupitia Filamu ya ITUNYAMA, na pia kupitia igizo la Jumba la dhahabu alizofanya akiwa chini ya director Tuesday Kihangala “Mr Chuzi”. Akizungumzia maisha yake ya ustaa, Snura anasema kuwa huwa anaumizwa sana pale anapoona habari kwenye vyombo vya habari zinazomuhusu ambazo mara nyingi anasema huwa si za kweli. Katika maisha yake ya kila siku Snura hupendelea sana kukaa ndani na kutazama Filamu mbalimbali kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment