Thursday, September 11, 2014

MAVAZI YA MABINTI WA CHUO, NGONO INAHAMASISHWA



Serikali ikiwa inaendelea kupiga vita kuhusu mavazi katika jamii yetu tunayo ishi hususani katika swala la kutunza maadili na utamaduni wa kitanzania bado swala la mavazi yanayovaliwa na vijana wa kitanzania hayaridhishi. Mbali na sheria zilizo wekwa hivi karibuni ambazo zina ambatana na ukiukwaji wa mavazi yanayo valiwa pamoja na kuweka adhabu, faini au vyote lakini sheria hizi hazifanyi kazi. Wahenga wanasema mguu huvunjika ikiwa la mkuu halija sikilizwa sasa tujiulize hilo la mkuu ambalo halija sikilizwa wangapi guu zao zimekwisha vunjika.

Ukiachana na wakazi wa mtaani sheria hizi za mavazi zinakaziwa sana vyuoni maana ndiko tunategemea hawa wasomi baadae ndio watakao kuja kuwa viongozi wa baadae na wazazi pia, Je vipi swala la mavazi vyuoni lina fuatiliwa ipasavyo…? Wanachuo wengi mavazi yao hayaridhishi hasahasa kwa upande wa dada zatu maana ndio wengi wao wasema “tunaenda na fashion”. Fashion ambayo inawalizimu wavae nusu utupu au ni kisingizio, hapa tunakuja kugundua ni uhuru wanao upata maana wengi ni wakazi wa mikoani sasa wanapo fika ugenini kule wasiko julikana ndio chimbuko hili hukua na kuathiri na wengine.
Imekuwa kawaida ukipita mtaani kusikia “Aahh wasichana wa chuo ni Malaya” kwa kuwa mavazi wanayo vaa hayana tofauti na yale wanayovaa dada zetu wanao fanya biashara ya mwili ilo moja, Pili kwa wanaume ambao hupenda mabinti wa aina hiyo hujikuta wanavutiwa nao na hapa sasa mabint wa chuo wanafananishwa na ATM kwa maana kuwa ni sehemu ya  kutolewa pesa za muhusika kwa ajili ya matumizi yao tofauti. Unadhani kuhakikisha wana endelea kuvaa nguo za aina hizo ambazo ziko nje na bajeti za wazazi wao ama walezi zinatoka wapi, wanajikuta wanajirahisisha kwa wanaume ili tu waendelee kushindana kimavazi na wenzao wanapokutana chuoni.

Elimu inahitaji kuwa makini na kusoma pia kitabu hakihitaji mtu mwenye mambo mengi kwa maana ndio unatengeneza msingi wa maisha ya baadae, kwa mwenendo ambao dada zetu wanaendelea nao si rahisi mtu wa aina hiyo kuwa makini na masomo mwisho wazazi wanakuwa wamewekeza pesa zao kwenye kampuni hewa.

0 comments:

Post a Comment