Thursday, July 10, 2014

RUFAA YA SUAREZ FIFA YAIKATAA



Shirikisho la soka Duniani FIFA limekatalia mbali ombi la rufaa la mchezaji wa Uruguay Luis Suarez dhidi ya marufuku yake ya mizi minne kwa kosa la kumng'ata Mlinzi wa Italia .
Katika barua kwa wanahabari FIFA ilisema kuwa imekatialia mbali ombi la Shirikisho la Soka la Uruguay la kuitaka kupunguza adhabu ya Mshambulizi huyo wa Liverpool .
Hata hivyo Suarez anauhuru wa kukata rufaa katika mahakama ya rufaa ya michezo (Court of Arbitration for S port) iwapo hataridhika na Uamuzi huo.
Mshambulizi huyo wa Liverpool alibanduliwa nje ya kombe la dunia baada ya tukio hilo la Juni tarehe 24 na sasa anaomba msamaha ili iwe rahisi kwake angalau kujifua pamoja na wachezaji wenza huko Anfield Uingereza huku akitarajia uhamisho kuelekea Uhispania katika klabu ya Barcelona .
Tukio hilo lilikuwa la tatu kwa mshambulizi huyo bora msimu uliyopita huko Uingereza.

0 comments:

Post a Comment