Thursday, July 10, 2014

BRAZIL KIWANDA CHA SAMSUNG KUVAMIWA


Simu 40,000 na mali zenye thamani ya dola milioni thelathini na sita zaibiwa.

Huko Brazil kombe la Dunia likiendelea kurindima kiwanda cha kampuni ya simu aina ya Samsung chavamiwa na wezi huku takribani simu 40,000 , tarakilishi pamoja na vifaa vingine kuripotiwa vimeibwa na wezi hao. Majira ya usiku siku ya Jumatatu wezi walivamia kiwanda cha simu cha Samsung nchini Brazil na kuiba mali yenye thamani ya dola milioni thelathini na sita.
Kundi la wezi lililo vamia kiwanda hicho tayari lilikuwa limesha jihami na kujipanga vikali dhidi ya tukio hilo wafanyakazi wane waliokuwa wakitoka kazini walitekwa na kuporwa vitambulisho vyao ambavyo walivitumia kuweza kingie ndani kama wafanya kazi wa kiwandani hapo kilichopo  mjini Sao Paulo, kutokana na kujipanga kwa kundi hilo la wezi imeripotiwa kuwa waliwazidi nguvu walinzi na kutumia muda wa saa tatu kufanya uhalifu.
Polisi wanasema kuwa genge hilo lilikuwa na wezi, 20 ambao walifanikiwa kuiba simu 40, 000 pamoja na tarakilishi, tabiti na vifaa ningine vyenye thamani ya dola milioni 36, walipovamia kiwanda hicho waliamuru wafanyakazi wote kuondoa betri zao kwenye simu ili wasiweze kumpigia mtu yeyote simukitendo kilichowaruhusu kutumia masaa matatu kufanya uhalifu huo na walifahamu vyema ambako vifaa vyenye thamani zaidi vilipokuwa vimewekwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa na kwamba kampuni hiyo haina tatizo lolote kwa sasa.Polisi wanachunguza kanda za video kuona ikiwa wanaweza kuwatambua wezi hao.

0 comments:

Post a Comment