Thursday, July 10, 2014

NEYMAR HOI, MUUGUZI AFUKUZWA





Muuguzi wa Hospitali ya Fortaleza Sao Paulo, Brazil  aliyopelekwa Neymar baada ya kuumia wakati wa mechi ya Brazil dhidi ya Colombia amefukuzwa kazi kwa kitendo chake cha kupiga picha za video wakati akiwasili hapo na kuzirusha kwenye mitandao ya kijamii. Picha hizo za video zilimwonyesha nyota huyo wa Brazil akipokelewa na kukimbizwa kwenye varanda za hospitali hiyo na madaktari zilionekana muda mfupi kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kutoka kwa taarifa kuwa Neymar hatoweza kucheza mechi zote zilizobaki za Kombe la Dunia.

Muuguzi huyo alijulikana kwa sababu mwisho wa video hiyo  aligeuza kamera upande wake na kusema “woo-hoo!” na kuonyesha tabasamu wakati nchi nzima ikiwa kwenye majonzi, pamoja na kushinda 2-1.
 Kwa mujibu wa Globo, uongozi wa hospitali umethibitisha kumfukuza muuguzi huyo kwa kitendo chake cha kuingilia maisha binafsi ya mgonjwa, wakati huohuo; Fifa haitochukua hatua yoyote dhidi ya beki wa Colombia aliyemuumiza Neymar, Fifa ilisema kamati ya nidhamu ilikaa na “hakuna haja ya kuchukua  hatua kwa tukio hilo’’ kwa sababu mwamuzi wa mechi hakuona wakati Camilo Zuniga akimgonga na kuchukua uamuzi kwa wakati


0 comments:

Post a Comment