Wednesday, October 22, 2014
TANZANIA KUPATA NEMBO YAKE YA BIASHARA
By Blog Hi5 at 8:47 PM
No comments
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tan Trade), ipo katika mchakato wa kuandaa nembo ya kibiashara itakayoitambulisha na kuitangaza Tanzania katika suala zima la uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika mkutano wa mchakato wa kupata usajili wa kuwa na nembo mpya ya Taifa, Mkurugenzi wa Tan Trade, Jacqueline Maleko, alisema kuwa ni vema ifikapo mwakani wakapata usajili utakaosaidia taifa kuwa na nembo yake.
Alisema endapo watafanikiwa kupata usajili Tanzania itatangazika katika uwekezaji na kwamba hakuna nchi itakayoweza kujitambulisha kibiashara kwa kutumia rasilimali za taifa.
Maleko aliongeza kuwa Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo pia ni adimu kupatikana katika nchi nyingine yeyote duniani na kwamba baadhi ya nchi zikifanya upotoshaji wa makusudi na kujitangaza kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini.
Aliongeza kuwa licha ya mchakato kuwa na changamoto zake kwa kuhitaji fedha nyingi mamlaka yake itahakikisha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanafanikisha suala hilo alilolitaja kuwa ni kilio chao cha muda mrefu.
Maleko alisema katika kuhakikisha wanafanikiwa katika azma hiyo ya kupata nembo ya Taifa ya kibiashara mamlaka yake itashirikiana na kampuni ya Squire Patton Boggs kutoka nchini Marekani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania (TPSF), Geofrey Simbeye alisema nchi imechelewa kupata nembo ya taifa na kwamba suala hilo lilipaswa kufanywa miaka 10 iliyopita na kuwataka wadau kuhakikisha suala hilo
MADEREVA, MAKONDAKTA UDA KUKIONA
By Blog Hi5 at 8:43 PM
No comments
ABIRIA wa mabasi jijini Dar es Salaam, wameshauriwa kusaidia kudhibiti uendeshaji holela na tabia zisizokubalika zinazofanywa na baadhi ya madereva na makondakta kwa kupiga simu zilizochapishwa katika mabasi yote ya Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA).
Taarifa ya UDA iliyotolewa jijini Da es Salaam jana na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, George Maziku, ilieleza kuwa utumiaji wa namba hizo utaisaidia pia kampuni kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja wake.
“Tunawakumbusha wateja wetu pamoja na watumiaji wengine wa barabara kuripoti uzembe wowote au utovu wa nidhamu utakaofanywa na madereva na makondakta wa UDA, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
“Mbali na kuboresha utoaji wa huduma zetu, UDA inalenga kuwa mfano wa kuigwa kwa mabasi mengine ya abiria nchini katika uzingatiaji wa sheria, utoaji wa huduma nzuri kwa wateja na kuwa kichocheo cha kupunguza foleni katikati ya jiji la Dar es Salaam,” alisema.
Maziku alisema uongozi wa UDA utachukulia kwa uzito mkubwa na kuyafanyia kazi maoni yote yakayokuwa yakitolewa kupitia namba hizo, ili kuondokana na dhana potofu kwamba wamiliki na waendeshaji wa kampuni za magari ya abiria ni watu ambao hawajaelimika.
Alisema mbali na uwepo wa namba hizo za simu, UDA itaendelea na utekelezaji wa utaratibu wake wa kutuma waratibu kupanda mabasi ya kampuni hiyo na kuripoti juu ya utendaji kazi wa madereva na makondakta wa mabasi hayo.
Tuesday, October 21, 2014
DIAMOND ANASWA AKIWA KITANDANI NA WEMA
By Blog Hi5 at 5:16 AM
No comments
NEW OFFICIAL VIDEO LIL WYNE_KRAYZ
By Blog Hi5 at 5:08 AM
No comments
DIAMOND PLATNUM SERENGETI FIESTA FULL SHOW
By Blog Hi5 at 4:56 AM
No comments
SERENGETI FIESTA 2014 TANGA_ALI KIBA
By Blog Hi5 at 4:46 AM
No comments
Monday, October 13, 2014
NEW BONGO MUVIE NA UJIO WA VISUALIZED EFX
By Blog Hi5 at 8:26 PM
No comments
Kutoka Visualized EFX, siku chache zilizopita walikuwa location wakifanya mazoezi ya kushuti falamu mpya inayohusu maisha ya kijana aliye rithishwa uchawi kimakosa kulingana na jinsi anavyo utumia katika mazingira anayoishi. Bloger wetu alipata nafasi ya kwenda kushuhudia zoezi hilo na pia aliongea na uongozi ambao haukuwa tayari kuzungumza chochote juu ya filamu hiyo kwa kuwa ndio kwanza ipo katika maandalizi na kusema chochote itakuwa mapema kuwajulisha wadau wa VEFX. Pia waliongezea kwa kusema wanahita kufanya vitu tofauti na ndio maana wanachukua muda mrefu kuandaa kazi zao mbali na hilo uchache wa vifaa wanavyo hitaji kufanyia kazi.
Moja kati ya assistance director pia ndiye mtunzi filamu za Visualized EFX Mr. Jackson a.k.a Jackcty alizungumza machache kuhusu kazi zinazo kuja mbeleni kuwa kuna kipindi kinafanyiwa final editing then soon kitakuwa kwa mtandao pia wadau wafahamu ya kuwa kampuni haina kazi moja tu ya kuandaa filamu ni pamoja kushuti vipindi, matangazo ya pamoja na event mbalimbali kwahiyo wadau wajiandae kupokea mengi kutoka VEFX.
“Tasnia ya Bongo movie ina changamoto nyingi kama Visualized EFX tunaandaa wasanii ambao watakuwa chini ya kampuni ya VEFX ambayo ni tawi la Akonshaz Music Co, na mara nyingi tunapenda kuandaa kazi zetu kwa wasanii ambao wako na malengo na ndio maana mpaka sasa ziko demo tu ambazo hivi karibuni mtazipata katika chombo cha habari cha Hi5 Media”hayo yalikuwa ni maneno yake mkuu wa kitengo kutaka Visualized EFX.