MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tan Trade), ipo katika mchakato wa kuandaa nembo ya kibiashara itakayoitambulisha na kuitangaza Tanzania katika suala zima la uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika mkutano wa mchakato wa kupata usajili wa kuwa na nembo mpya ya Taifa, Mkurugenzi wa Tan Trade, Jacqueline Maleko, alisema kuwa ni vema ifikapo mwakani wakapata usajili utakaosaidia taifa kuwa na nembo yake.
Alisema endapo watafanikiwa kupata usajili Tanzania itatangazika katika uwekezaji na kwamba hakuna nchi itakayoweza kujitambulisha kibiashara kwa kutumia rasilimali za taifa.
Maleko aliongeza kuwa Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo pia ni adimu kupatikana katika nchi nyingine yeyote duniani na kwamba baadhi ya nchi zikifanya upotoshaji wa makusudi na kujitangaza kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini.
Aliongeza kuwa licha ya mchakato kuwa na changamoto zake kwa kuhitaji fedha nyingi mamlaka yake itahakikisha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanafanikisha suala hilo alilolitaja kuwa ni kilio chao cha muda mrefu.
Maleko alisema katika kuhakikisha wanafanikiwa katika azma hiyo ya kupata nembo ya Taifa ya kibiashara mamlaka yake itashirikiana na kampuni ya Squire Patton Boggs kutoka nchini Marekani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania (TPSF), Geofrey Simbeye alisema nchi imechelewa kupata nembo ya taifa na kwamba suala hilo lilipaswa kufanywa miaka 10 iliyopita na kuwataka wadau kuhakikisha suala hilo
0 comments:
Post a Comment