• This is Slide 1 Title

    This is slide 1 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 2 Title

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 3 Title

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Thursday, July 10, 2014

WANNE WAUWAWA KATIKA AJALI YA NDEGE NAIROBI

WAWILI KUWAHISHWA HOSPITALI WAKIWA MAJERUHI


Watu wanne wameripotiwa kuuwawa asubuhi ya Jumatano baada ya ndege ya mizigo kuanguka katika mtaa wa Utawala mjini Nairobi na kusababisha uharibifu wa majengo mawilli kabla ya ndege hiyo kuanza kuwaka moto
Mbali na ndege hiyo kusababisha vifo vya watu wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo akiwemo na rubani aliye kuwa akipaisha ndege hiyo chanzo cha habari kinaeleza kuwa walio kuwa walinzi wa majengo mawili yaliyo haribiwa na ajali hiyo nao ni majeruhi na wapo hospitali kwa matibabu. Benson Kibue ambaye ni mkuu wa Polisi wa County ya Nairobi amesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi alfajiri wakati ndege hiyo ya shirika la Skyward kuanguka na kuwaka moto.
Ajali hiyo ya ndege ya mizigo inayomilikiwa na shirika la Skyward, iliyokowa ikisafirisha mzigo ilipata ajali muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa Kimataifa wa Kenyataa mjini Nairobi iliyo kuwa ikisafirisha Mirungi kutoka Kenya kuelekea Mogadishu, Somalia ndiyo iliyo chukua uhai wa raia wanne akiwemo rubani mmoja na kujeruhi walinzi wawili huko mjini Nairobi.

49 WAUWAWA BAADA YA NDEGE YA UKRANE KUTUNGULIWA




Wizara ya ulinzi inasema ndege hiyo ilikuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Luhansk, Maafisa wa Ukraine wanasema  watu wanaopigana kujitenga na kujiunga na  Russia, wametungua ndege ya uchukuzi ya kijeshi na kuuwa watu wote 49 waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Ofisi ya mwendesha mashataka mkuu huko Ukraine, ilisema wanajeshi 40 na wafanyakazi tisa waliuawa mapema leo Jumamosi  baada ya ndege hiyo ya jeshi la angani la Ukraine kupigwa risasi na kuanguka. Wizara ya ulinzi inasema ndege hiyo ilikuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Luhansk ilipopigwa risasi. Ukanda wa video  unaonyesha mlipuko mkubwa karibu na uwanja huo wa ndege, unaoaminika kutoka kwa ndege  hiyo.

RUFAA YA SUAREZ FIFA YAIKATAA



Shirikisho la soka Duniani FIFA limekatalia mbali ombi la rufaa la mchezaji wa Uruguay Luis Suarez dhidi ya marufuku yake ya mizi minne kwa kosa la kumng'ata Mlinzi wa Italia .
Katika barua kwa wanahabari FIFA ilisema kuwa imekatialia mbali ombi la Shirikisho la Soka la Uruguay la kuitaka kupunguza adhabu ya Mshambulizi huyo wa Liverpool .
Hata hivyo Suarez anauhuru wa kukata rufaa katika mahakama ya rufaa ya michezo (Court of Arbitration for S port) iwapo hataridhika na Uamuzi huo.
Mshambulizi huyo wa Liverpool alibanduliwa nje ya kombe la dunia baada ya tukio hilo la Juni tarehe 24 na sasa anaomba msamaha ili iwe rahisi kwake angalau kujifua pamoja na wachezaji wenza huko Anfield Uingereza huku akitarajia uhamisho kuelekea Uhispania katika klabu ya Barcelona .
Tukio hilo lilikuwa la tatu kwa mshambulizi huyo bora msimu uliyopita huko Uingereza.

NDEGE YA MALYASIA VIFAA KUONEKANA BAHARI YA HINDI



Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott ameliambia bunge kwamba picha za setaliti zinaonesha vifaa vinavyo fanana na mabaki ya ndege ya Malyasia iliyopotea nje ya pwani ya kusini magharibi ya Australia katika eneo kusini ya Bahari ya HIndi.
Bw. Abbott anasema ndege ya kijeshi imepelekwa katika eneo hilo na inatazamiwa kuwasili Alhamisi mchana saa za Austrlia, na ndege nyingine tatu zitapelekwa kuanza uchunguzi wa kina kutafuta eneo hilo.
Hata hivyo Bw Abbot alionya kwamba kazi za kutafuta na kupata vyombo hivyo inaweza kua ngumu na huwenda visihusiane na ndege hiyo nambari MH370.

DIAMOND PLATNUM MDOGO MDOGO (OFFICIAL VIDEO)


Kama alivyo ahidi mashabiki wake wiki chache kupita ataachia mizigo sumu kwa hewa sasa deni limelipwa kwa kishindo, kutoka mitandao tofauti Diamond Platnum amekwisha achia vichupa vyake kikiwepo Mdogo mdogo pamoja na alicho fanya na Iyanya huko Nigeria where by Audio produced by Tudy Tomas kwenye Video mtu mzima The Director Mr. Moe Musa kwenye kichupa cha Bum Bum

 DIAMOND PLATNUM-MDOGOMDGO OFFICILA VIDEO



Video ya nyimbo aliyo mshirikisha kinara wa Nigeria Iyanya, BumBum

DIAMOND PLATNUM FT. IYANYA-BUMBUM


WEMA SEPETU, KAJALA MASANJA BIFF KUSHNEY!!



Muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu, amesema amefurahi kurudiana ‘ushosti’ na muigizaji mwenzake, Kajala Masanja, Wema alisema pamoja na Kajala kumkosea ila amefurahi kuwa naye karibu kwani alikuwa anakwazika na hasa alipokuwa anasikia habari zake kwa watu wa karibu na Kajala.
“Nashukuru Mungu hili bifu limeisha kiukweli, nimefurahi sana kwani nilikuwa nakwazika kila nikipata habari za Kajala kwa watu wake wa karibu, kiukweli nimefurahi,” alisema Wema.
Wema Sepetu na Kajala walikuwa na bifu lililokuwa linadhaniwa haliwezi kumalizika hadi kufikia hatua ya kuundwa kwa makundi yanayodaiwa ya kiuchochezi baina yao.