Wednesday, April 27, 2016

POLISI ABAKA MWANAFUNZI


Mwanafunzi wa kidato cha tatu, juzi alimkaanga askari polisi anayedaiwa kumbaka kwa kuieleza Mahakama jinsi alivyotendewa kitendo hicho katika kibanda cha ulinzi cha benki.

Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Misungwi, Ruth Mkisi, shahidi huyo alidai siku ya tukio askari huyo, Raphael Sixstus (30), alimuita alipokuwa akipita karibu na Benki ya CRDB Tawi la Misungwi, alipoitikia wito ghafla alivutiwa ndani ya kibanda hicho na kumbaka.
“Wakati akinitendea kitendo hicho, alikuwa akinitishia kisu huku akiniambia nikipiga kelele ataniua, niliogopa nikaa kimya ingawa niliumia na kutokwa damu nyingi sana,” alidai shahidi huyo.
Akiongozwa na Mwendasha Mashtaka wa Polisi, Doreth Mgenyi, mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16 alidai kabla ya kumbaka, mshtakiwa huyo alimvua nguo zote za ndani.
Awali, Mwendesha mashtaka alipokuwa akimsomea makosa mshtakiwa huyo alidai kuwa Novemba 20, mwaka jana, akiwa eneo la lindo katika Benki ya CRBD Tawi la Misungwi, alimbaka mwanafunzi huyo saa 1.00 usiku wakati akitoka mashine kusaga unga katika maeneo ya Bomani.
Hakimu Mkisi aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa kwa upande wa mashtaka kuita mashahidi wengine. Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana.

Related Posts:

  • UKIMYA WA UPINZANI BUNGENI MASHAKA KWA WASOMI UAMUZI wa Kambi ya Upinzani bungeni kuingia katika vikao vya Bunge na kugeuka bubu wakati wa mjadala wa Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, umechukuliwa kwa hadhari kuwa unaweza kusababisha kambi hiyo ionekane inalinda posho bu… Read More
  • Wakenya kinara katika London Marathon Mwanariadha mkenya Eliud Kipchoge nusura avunje rekodi ya duniaya mbio za Marathon alipoandikisha muda wa kasi zaidi katika mbio za London Marathon. Kipchoge wa Kenya,alihifadhi taji aliloshindwa mwaka uliopita alipoandikish… Read More
  • Serikali ya China kudhibiti dini Chama cha kikoministi cha China kimepewa mamlaka ya kudhibiti dini nchini humo. Kiongozi wa Uchina, Xi Jinping, amesema makundi ya kidini lazima yakubali kudhibitiwa na chama cha kikoministi. Akizungumza katika mkutano wa s… Read More
  • NAPE AZINDUA TAMASHA LA KIMATAIFA LA FILAMU MJINI ARUSHA  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani Arusha .  Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu wali… Read More
  • TWITTER YAMTIA NDANI MWANDISHI Polisi nchini Uturuki wamekamata mwandishi wa habari aliyemkosoa rais wa nchi hiyo kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Ebru Umar raia wa Uholanzi alikamatwa na polisi baada ya kumkosoa rais Recep Tayyip Erdogan alikamatwa… Read More

0 comments:

Post a Comment