Serikali ikiwa inaendelea kupiga vita kuhusu mavazi
katika jamii yetu tunayo ishi hususani katika swala la kutunza maadili na
utamaduni wa kitanzania bado swala la mavazi yanayovaliwa na vijana wa
kitanzania hayaridhishi. Mbali na sheria zilizo wekwa hivi karibuni ambazo zina
ambatana na ukiukwaji wa mavazi yanayo valiwa pamoja na kuweka adhabu, faini au
vyote lakini sheria hizi hazifanyi kazi. Wahenga wanasema mguu huvunjika ikiwa
la mkuu halija sikilizwa sasa tujiulize hilo la mkuu ambalo halija sikilizwa
wangapi guu zao zimekwisha vunjika.
Ukiachana na wakazi wa mtaani sheria hizi za mavazi
zinakaziwa sana vyuoni maana ndiko tunategemea hawa wasomi baadae ndio watakao
kuja kuwa viongozi wa baadae na wazazi pia, Je vipi swala la mavazi vyuoni lina
fuatiliwa ipasavyo…? Wanachuo wengi mavazi yao hayaridhishi hasahasa kwa upande
wa dada zatu maana ndio wengi wao wasema “tunaenda na fashion”. Fashion ambayo
inawalizimu wavae nusu utupu au ni kisingizio, hapa tunakuja kugundua ni uhuru
wanao upata maana wengi ni wakazi wa mikoani sasa wanapo fika ugenini kule
wasiko julikana ndio chimbuko hili hukua na kuathiri na wengine.
Imekuwa kawaida ukipita mtaani kusikia “Aahh
wasichana wa chuo ni Malaya” kwa kuwa mavazi wanayo vaa hayana tofauti na yale
wanayovaa dada zetu wanao fanya biashara ya mwili ilo moja, Pili kwa wanaume
ambao hupenda mabinti wa aina hiyo hujikuta wanavutiwa nao na hapa sasa mabint
wa chuo wanafananishwa na ATM kwa maana kuwa ni sehemu ya kutolewa pesa za muhusika kwa ajili ya matumizi
yao tofauti. Unadhani kuhakikisha wana endelea kuvaa nguo za aina hizo ambazo
ziko nje na bajeti za wazazi wao ama walezi zinatoka wapi, wanajikuta
wanajirahisisha kwa wanaume ili tu waendelee kushindana kimavazi na wenzao wanapokutana
chuoni.
Elimu inahitaji kuwa makini na kusoma pia kitabu
hakihitaji mtu mwenye mambo mengi kwa maana ndio unatengeneza msingi wa maisha
ya baadae, kwa mwenendo ambao dada zetu wanaendelea nao si rahisi mtu wa aina
hiyo kuwa makini na masomo mwisho wazazi wanakuwa wamewekeza pesa zao kwenye
kampuni hewa.
0 comments:
Post a Comment