Tanga ni mkoa mmoja wapo unaopatikana hapa Tanzania
ukiwa katika pwani ya Afrika mashariki ya Bahari ya Hindi. Ni kilometa mia tatu
Hamsini ukitokea (350 KM) Dar-es-salaam hadi Tanga. Mkoa huu kwakeli una mambo
mengi yakihistoria kati ya mikoa maarufu sana enzi hizo Tanzania huwezi kuacha
kuutaja mkoa wa Tanga. Team Hi5 Media ilifanikiwa kutembelea mkoa wa Tanga
ambapo ilitembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria ikiwemo bandari kongwe ya
Tanga, Mapango ya Amboni na kiwanda cha maziwa mpaka kule kwenye magofu ya
kihistoria na katika kile kisiwa ambacho kinazama kinacho itwa Tongoni.
“YES GOOD BYE” ni maneno yaliyo tumiwa na bwana
Osali Otango pindi alipokuwa akihudhuria mikutano ya wazungu pia alikazia kwa
kusema “YOU WILL NEVER” pale wazungu wakikoloni walipo jadiliana jinsi ya
kumkamata bwana huyu Osali Otango. Osali Otango alikuwa ni gwiji katika matumizi
ya nguvu za giza mara zote alitafutwa na wakoloni wakizungu bila kupatikana. Osali
Otango aliishi sehemu ya miujiza sehemu yakihistoria sehemu yenye mambo mengi
ya kustaajabisha ambayo miaka milioni ishirini nyuma nazungumzia mapango ya amboni
ama kwa jina la kisasa Amboni Caves. Mapango haya kwa sasa ni kivutio kikubwa
cha utalii hapo mkoani Tanga. Katika mapango haya kuna mahali ambako watu
walipatumia kuabudu na kufanya kafara wengi wao walikuwa ni makabila yanayo
zunguka mapango haya yaani wazigua, wabondei pamoja na wadigo hapo zamani.
Katika mapango haya kuna miamba inayo toka chini kwenda juu na inayotoka juu
kuja chini kwa lugha ya kitaalamu wanajografia huita Slack tight na slug might
pia kuna miamba inayo kutana na kutengeneza aina nyingine kabisa ambyo wanaiita
Earth Pira.
Wanasema ukiyastaajabu ya musa utayaona ya firauni
ndani ya mapango haya pana maumbo ya kijinsia, jinsia ya kike na jinsia ya
kiume, pia kuna kiti cha asili kilicho chongwa na maji pamoja na kwato lakini
pia ndani ya mapango haya kuna eneo ambalo dini ya kiislam na dini ya kikristo
walikuwa wakipatumia kwa ajili ya kufanya ibada ama hakika mapango haya ni
kivutio kikubwa sana.
Imeandikwa na Donald Mtani “The Super Voice” Hi5
Makala
0 comments:
Post a Comment