Monday, April 25, 2016

SERA YA ELIMU BURE YATOLEWA UFAFANUZI


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewataka walimu na maafisa elimu kusimamia vyema majukumu yao na kuhakikisha utoaji elimu bora kwa wanafunzi ili kupata wataalamu watakaolisaidia taifa.

Waziri Ndalichako, ameyasema hayo Jijini Arusha, alipokutana na wakuu wa shule,maafisa elimu na watendaji wakuu wa idara za elimu ambapo amesisitiza nidhamu ili kusaidia matokea mazuri na ya haraka ya kuboresha elimu nchini.
Waziri Ndalichako, amesema kuwa wataalamu mbalimbali ambao wanahitajia katika idara mbalimbali katika kukuza maendeleo wote wanahitaji zaidi mchango wa sekta ya elimu katika kuwapata wataalamu hao.
Aidha katika ziara aliyoifanya katika mkoa huo wa Arusha, Waziri Ndalichako, ametoa ufafanuzi zaidi wa sera ya elimu bure ambapo amesema kuwa wazazi bado wanajukumu la kushirikiana na serikali katika kuwasadia watoto kupata elimu bora.
Prof. Ndalichako amesema serikali haijawazuia wananchi wanaotaka kuchangia sekta ya elimu kutokana na changamoto zilizopo lakini haiko tayari kuona mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa sababu ya michango ya aina hiyo.

Related Posts:

  • NAPE AZINDUA TAMASHA LA KIMATAIFA LA FILAMU MJINI ARUSHA  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani Arusha .  Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu wali… Read More
  • Wakenya kinara katika London Marathon Mwanariadha mkenya Eliud Kipchoge nusura avunje rekodi ya duniaya mbio za Marathon alipoandikisha muda wa kasi zaidi katika mbio za London Marathon. Kipchoge wa Kenya,alihifadhi taji aliloshindwa mwaka uliopita alipoandikish… Read More
  • Serikali ya China kudhibiti dini Chama cha kikoministi cha China kimepewa mamlaka ya kudhibiti dini nchini humo. Kiongozi wa Uchina, Xi Jinping, amesema makundi ya kidini lazima yakubali kudhibitiwa na chama cha kikoministi. Akizungumza katika mkutano wa s… Read More
  • Serikali ya China kudhibiti dini Chama cha kikoministi cha China kimepewa mamlaka ya kudhibiti dini nchini humo. Kiongozi wa Uchina, Xi Jinping, amesema makundi ya kidini lazima yakubali kudhibitiwa na chama cha kikoministi. Akizungumza katika mkutano wa s… Read More
  • UKIMYA WA UPINZANI BUNGENI MASHAKA KWA WASOMI UAMUZI wa Kambi ya Upinzani bungeni kuingia katika vikao vya Bunge na kugeuka bubu wakati wa mjadala wa Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, umechukuliwa kwa hadhari kuwa unaweza kusababisha kambi hiyo ionekane inalinda posho bu… Read More

0 comments:

Post a Comment