• This is Slide 1 Title

    This is slide 1 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 2 Title

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • This is Slide 3 Title

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Sunday, August 31, 2014

JAY DEE KOMANDO ATOLEA UVIVU MAGAZETI YA UDAKU





Iko haja ya kuzingatia magazeti yanayo andika vitu visivyo na uchunguzi yakinifuu juu ya habari zinazotolewa. Hivi karibuni gazeti moja limeandika habari kumhusu Komando Lady Jay Dee ambazo hazikumfuraisha ndipo alipo amua kuonyesha ukomando wake kwa kufunguka juu ya ukweli wa habari ya kuwa ana toka na dogodogo. Kupitia mtandao wa kijamii Komando Jay Dee alifunguka yafuatayo…
“Zamani ilikuwa haipo sehemu ya kujitetea, gazeti likishaandika ndio limeandika. 
Lakini sasa ulimwengu umebadilika, sio muda wa watu wote kulishwa chakula kisichofaa. 
Kwanza hicho kichwa cha habari kimenivunjia heshma sana. Nafikiri lengo ni kuilazimisha jamii inayomuelewa JayDee tofauti imuone kuwa ni mtu asiefaa, sawa. Dogo anaswa na mkoko? Huo mkoko mmemnasa nao wapi wakati hizo picha ni mimi nilizi post mwezi February Instagram?
Picha ambazo zilipigwa Nyumbani lounge tena kutumia simu ya Gardner.
Jide, dogodogo gumzo mjini. Gumzo ni kitu kinachoongelewa sana na kilichoenea kila kona sasa hii habari ni gumzo wapi ambapo haisikiki.

Mngeandika tumeamua kumuanzishia Jide gumzo hili, ndio ningewaelewa. 
Vitu vya kuzua. Ni watu wengi tu wakija band wakipata nafasi wanaomba kupiga picha na mimi na wengine pia wanaomba kupiga picha na gari sababu wanaipenda. Kama mtu yoyote anavyoweza kupiga picha na sanamu la kitu chochote anachokipenda. Hivi je! Wimbo wa JayDee mgumba, JayDee tasa umechuja? Umeisha chati?? Nashangaa na najiuliza tu
Inawezekana wimbo huo umechuja ndio maana mnatafuta wimbo mwingine utakao hit zaidi ya ule. Ndio kinachopelekea kuandika story za namna hii. Sio nyinyi mliokuja kuomba radhi kwa yote mliowahi kuniandika na kudai kuwa mmejirekebisha, miezi kadhaa tu iliopita?
Sio boss wenu aliemfuata Gardner na kumwambia tumalize tofauti zetu? 
Kama hizo tofauti zilikuwepo Inawezekana nyie ndio mna tofauti na mimi, sijawahi kuwa na tofauti na mtu hata nisiemfahamu.

Nashukuru Mungu nilikataa msamaha wenu ni kama nilihisi hamkumaanisha au sababu sijawahi kukubali show mlizotaka kufanya na mimi? Je! Hiki ni kisasi? Sielewi Mungu alienisimamia ataendelea Hii sio vita ya kwanza wala ya mwisho Dunia ni mapambano.
Kama nia ni kufanya niishi maisha ya uoga, kudhoofika na msongo wa mawazo mmefeli wengine mkijidai ni wacha Mungu huku mkiumiza nafsi za watoto wa binadamu wenzenu. 
No wonder mnaishi bila amani mbali na utajiri mlionao kwa kuogopa visasi. Sikuzaliwa kukata tama pia wapo wanaopenda kuandikwa kwenye hayo magazeti yenu wafanyieni favor ya kuwapa hiyo nafasi mi sifanyi muziki wa magazeti ya udaku  mkiachana na mimi nitashukuru sana hata ndoa yangu ikivunjika haimaanishi mnitafutie story za kunichafua ndoa ya Madiba ilivunjika sembuse yangu nina utofauti ipi na binadamu wengine? Nyie ndoa zenu ziko perfect si ndio? 
Hewala watakatifu nyie, mnaoficha yenu na kutangaza ya wenzenu.

Mwisho nawaomba watu mnaonielewa kutoamini tu habari yoyote ambayo haijatoka kwangu wala kwa muwakilishi wangu ambae ni "Webiro Wakazi Wasira".
Kama kuna chochote cha watu kujua nitakiongea mimi kwa mdomo wangu sio kuwekewa maneno mdomoni. Kila siku ooooh tulimpigia simu hapatikani, namba yangu yenyewe kwanza hata mnaijua? Mngekuwa mnaijua msingekuwa mnahangaika mnawapigia watu wangu wa karibu kunitafuta , na hao watu hawawezi kunisaliti ndio sababu mpaka miaka 70 mtaishia kusema tulimpigia simu JayDee hapatikani. Nyie muongee chochote mnachojiskia Ila sie hatuna haki kujitetea? Hili nalo litapita kama mengine  Na inshallah nitakuwa hapa hapa nimesimama nawaangalia, Picha moja wapo ni hiyo ambapo mtoto wa vitoto alikuja siku hiyo hiyo na akapiga picha na Gardner, mbele ya gari hiyo hiyo mnayodanganya watu kuwa mmemkuta nayo na mahala ni hapo hapo Nyumbani Lounge, ,,,,, na picha nyingine ni hizo nilizowahi kuzi post mimi mwenyewe mwezi february leo zinanihukumu endeleeni kudanganya jamii Na hizo ni chat alizoniandikia huyo mtoto wa vitoto ambae ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona na sijawahi kumuona tena. . Zaidi ya kuongea nae twitter ,,, sisemi kama mimi malaika lakini
Ukweli huwa hauchanganywi na uongo Kwa hili mmenidhalilisha sana 
Kama nia yenu jamii inione mwanamke nisiefaa na ninaependa dogodogo Basi Mungu atawaonyesha ukuu wake”..

Friday, August 22, 2014

WAUAJI WA FORLEY MAREKANI YAWASAKA.



Ahadi ya Rais Barak Obama, Kuimarisha Ulinzi Marekani.
Kitengo cha sheria nchini Marekani kimeanza kufanya uchunguzi wa jinai dhidi ya kifo chamwandishi wa habari mwenye asili ya Marekani ,James Foley aliyeuawa na wapiganaji wa kiislamu wenye msimamo mkali. Mwanasheria mkuu wa kitengo hicho,Eric Holder ameweka wazi kuwa wote waliohusika na mauaji ya mwandishi huo watawatia mkononi muda si mrefu. Maofisa wa serikali ya Marekani wandai kwamba askari hao wauaji walidai kiasi kikubwa cha pesa zipatazo dola za kimarekani zaidi ya milioni mia moja na thelathini kama fidia ya kumuachilia James Foley.
Marekani imekwisha anza harakati za kuwasaka na hatimaye kuwakamata waliohusika na mauaji ya mwandishi huyo kwa kurusha ndege zake takriban sita katika anga inayomilikiwa na waislamu kaskazini mwa Iraq.pamoja na kwamba waislam hao kutishia kumuua mmarekani mwingine wanayemshikilia kama ulipizaji wa kisasi endapo mashambulio yataelemea upande wao.

AFISI ZA NFF ABUJA ZATEKETEA



Moto wateketeza afisi za NFF Abuja

Moto mkubwa umetekeza makao ya shirikisho la soka la Nigeria NFF iliyoko Abuja, moto uliowachukua zaidi ya saa mbili kuuzima huku wakisaidiana na umma kuuzima moto huo mkubwa . Afisa wa kuzima moto Eyo amesema kuwa wanashuku ya kwamba chanzo cha moto huo ulitokana na hitilafu ya umeme.
Katibu mkuu wa NFF bwana Musa Amadu amesema kuwa moto huo ulianzia katika afisi ya mhasibu wa shirikisho hilo.
"Niliwasili kama kawaida lakini nikakatazwa kupanda ghorofa kwani tayari moshi ulikuwa unafuka ''
"Wafanyikazi wa shirikisho hilo wangeweza kuzima moto huo lakini walishindwa kuingia ofisini humo na hivyo hawangfeweza kubaini chanzo kikamilifu''
''Hata hivyo nashukuru mungu kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha yake kutokana na moto huo kwahivyo hakuna faida ya kumlaumu mtu yeyote''
Mwenyekiti wa NFF Aminu Maigari anakumbwa na tuhuma za uongozi duni kutokana na mkasa huo wa moto ni pigo kwa shirikisho hilo ambalo tayari linakabiliwa na mvutano wa uongozi ambao umepelekea kung'olewa madarakani kwa mwenyekiti Aminu Maigari mara mbili akirejeshwa

KAMATI NDOGO YAUNDWA NA MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA




Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ameunda kamati ndogo yenye ujumbe wa watu 10 kwa ajili ya kushughulikia masuala ambayo  hayakufikia muafaka wakati wa majadiliano ya kupitia sura mbalimbali za Rasimu ya Katiba Mpya kwenye Kamati 12 za Bunge hilo.

Kamati hiyo itakuwa inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samia Suluhu Hassan,ambapo  wajumbe  wa kamati hiyo wametoka kila pande ya Muungano  yaani watano wametoka Tanzania Bara na watano kutoka Zanzibar.

Aidha Mhe. Sitta akizungumzia kuhusu  maendeleo  ya kazi za Kamati  hizo, ambapo alisema zinaendele vizuri, hivyo kuanzia wiki ijayo sura zote 15 zitakuwa zimepigiwa kura,hivyo  Kamati hizo zitakuwa zimemaliza sura 17 ya rasimu hiyo na za nyongeza ifikapo Agosti 27,mwaka huu  ili kuanza kuwasilisha katika Bunge hilo kuanzia Septemba 2,mwaka huu.


Hayo yalisemwa leo na  Mhe. Samuel Sitta wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao leo kuhusu muhtasari wa kikao cha Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo kilichokaa leo kutathmini kazi za Kamati 12 za Bunge hilo lilipofikia pamoja kuridhia baadhi ya mapendekezo ya kuongeza Ibara na sura ndani Rasimu ya Katiba katika Kamati zao.
Mwenyekiti huyo aliyataja mambo ambayo yatashughulikiwa na kamati hiyo, ni muundo wa  Bunge  katika masuala  ya Muungano, uraia pacha, mahakama ya kadhi na kamati ya pamoja ya fedha.
“Haya mambo manne nimeagiza ufanyike utaratibu maalum,” alisema Mhe. Sitta.

 Mhe . Sitta  akizungumzia kuhusu tathimini ya mwenendo wa Kamati hizo, alisema zipendekeza masuala kadhaa na kuacha mengine  kama yalivyo katika rasimu hiyo.

Akizungumzia kuhusu yaliyojadiliwa katika kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo,kabla ya kukutana na waandishi wa habari, Mhe. Sitta alisema kamati hiyo imepokea mapendekezo kutoka katika kamati mbalimbali kuhusu kuongezeka kwa sura na Ibara za rasimu hiyo.

Aliyataja mapendekezo hayo , likiwemo la  Tume ya Marekebisho ya Katiba lililowasilisha na Jaji Warioba kuhusu ardhi, mazingira na rasilimali za taifa, Jumuia ya Tawala  za  Serikali za Mitaa (ALAT) na pendekezo la Haki ya Watumiaji huduma na bidhaa ili kuwalinda walaji lililowasilishwa , Hawa Ng’umbi  ambaye ni mjumbe wa Bunge hilo.

Aliyataja  mapendekezo  mengine  ni la  Jukumu la Serikali kujenga uchumi imara, ambapo lengo ni kuwa na maendeleo ya uchumi wa ujamaa na kujitegemea na Kuwepo kwa Baraza la Habari, la wajumbe wa 201 kuhusu ardhi, wafugaji, wavuvi pia na wachimbaji wadogo ili ziweze kutungwa Sheria za kusimamia masuala hayo.


Mhe. Sitta  alisema kutokana na mapendekezo  hayo kutakuwepo na ongezeko la ukurasa na sura kadhaa katika rasimu hiyo.

Alisema Kamati imebaini tatizo la mahudhurio,  aliwapongeza wajumbe wa Bunge hilo kutoka upande wa Zanzibar kwa kuwa na mahudhurio mazuri kwenye vikao kuliko kutoka  Tanzania Bara kuacha visingizio vya kutohudhuria vikao.

Katika hatua nyingine Mhe. Sitta alisema kutakuwepo na wataalamu  kabla ua kumalizika  kwa wiki hii kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa mambo  kadhaa kutoka Hazina kwa pande zote za Muungano, ambapo ataukuwepo pia Gavana wa Benki Kuu, Profesa Bonaventure Rutinwa kwa ajili ya suala la uraia pacha, uhamiaji  na Profesa Issa Shivji ambaye ataoa ufafanuzi juu ya aina ya Muungano ili kuwa na uwiano kwa kuwa hivi sasa yapo mambo machache. Imeandikwa na Magreth Kinabo, Dodoma  

MARIO BALOTELLI RASMI LIVERPOOL.





Klabu ya Liverpool imemsajili rasmi mshambuliaji machachari Mario Balotelli kwa jumla ya kiasi cha paundi milioni 16. Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa wameamua kumchukua mshambuliaji huyo ili kuziba pengo lililoachwa wazi na Luis Suarez ambaye amehamia Barcelona. Balotelli ambaye mwaka jana alijiunga na timu ya AC millan kwa uhamisho wa paund milion 19 akitokea Machester City hadi sasa ameweza kufunga magoli 30 katika michezo 54. Balotelli alijiunga na Manchester City August 2010 kwa paundi milion 24 wakati huo akitokea Inter Milan ambako aliiwezesha klabu yake kuchukua kombe katika michuano ya ligiya England.