Monday, April 25, 2016

PICHA ZA UCHI ZAMFUNGA SIWEMA WA NEY WA MITEGO



Wiki iliyopita zilianza kusikika taarifa mbalimbali kuhusu kuhukumiwa kwa mpenzi wa zamani na mama mtoto wa msanii Nay wa Mitego aliyehukumiwa kwenda jela miaka miwili  jijini  Mwanza.

Pamoja na taarifa zote hizo kutoka hakukuwa na taarifa za kina kuelezani nini hasa kilitokea mahakamani mpaka akahukumiwa jela miaka miwili  ila taarifa za awali  zilidaikwamba amehukumiwa kwa sababu ya kutukana mtu mtandaoni.
Wakili wa serikali Moris Mtoi ameongea kwenye exclusive interview na DStv  na kusema ukweli au chanzo cha Siwema kuhukumiwa hakikua kumtukana mtu mitandaoni bali kumtishia mtu.
Amesema kilichompeleka Siwema jela ni kumtishia mpenzi wake wa zamani kutoa picha za uchi walizopiga, Siwema alikua akimtishia kwamba asingetoa pesa na kumnunulia gari au kufata maagizo yake angezisambaza picha hizo kwa mke wake na watu wengine.
Wakili huyu wa serikali na mwendesha mashtaka kwenye kesi hii amesema vitu vingine alivyokuwa akivitaka Siwema ni kununuliwa nyumba na boyfriend wake huyu wa zamani.

0 comments:

Post a Comment